Tuesday 9 January 2018

WAZAZI WAMTUHUMU MWL MKUU S/M KWA KUWAFUKUZA WANAFUNZI NA KUWATOZA MICHANGO

DSC_0261
Moja kati ya madarasa ya shule ambayo  mkuu wake analalamikiwa na wananchi kuwatoza michango mbali mbali.

Wazazi na walezi wa mtaa wa Moringe Kata ya Buhalahala Wilayani Geita wamemtuhumu mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya 14 kambarage kwa kuwarudisha wanafunzi nyumbani kutokana na kutotoa fedha za mchango shuleni hapo.


Tangu Serikali ya awamu ya tano iingie madarakani chini ya Rais Dr John Pombe Magufuli kupitia wizara ya elimu, sayansi na ufundi ilitoa waraka wa elimu bure kuanzia elimu ya msingi mpaka kidato nne.


Akizungumzana Storm  HABARI , Bi Odest Timoth alisema kuwa wamekuwa wakitozwa fedha pindi wanapopeleka watoto wao kuwaandikisha na wanapogoma kutoa wamekuwa wakirudishwa na Mkuu wa shule  na huku wanatambua kuwa serikali imetoa kibali cha wanafunzi kusoma bure bila ya kutoa pesa hivyo hali hiyo imeendelea kuwachanganya.


“Hali hii  sio nzuri kabisa serikali imesema watoto wasome bure leo hii wazazi tunalazimishwa kutoa michango tena pindi tu unapopeleka mtoto mimi naomba mkuu wa wilaya hatusaidie juu ya huyu mwalimu maana imeshakuwa ni kero”alisema Bw Peter John .


Diwani wa Kata ya Buhalahala Bw Mussa Kabese  alisema amekuwa akipokea simu za wazazi wakimlalamikia Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi 14 Kambarage kuwaomba wazazi kiasi cha shilingi elfu kumi na pindi wanaposhindwa kutoa amekuwa akiwafukuza watoto shuleni hapo jambo ambalo sio sahihi.


Kufuatia tuhuma hizo mtandao huu umemtafutta Mwalimu Mkuu Jacob Bossco ambaye ni mwalimu mteule wa kusimamia shule hiyo akitokea shule ya msingi Mbugani ambapo , amekanusha  kuhusika na tuhuma hizo na kuelekeza tuhuma hizo kwa kamati ya ujenzi pamoja na ofisi ya Serkali Mtaa wa 14 Kambarage.


Kutokana na madai hayo Mkuu  wa Wilaya Mwl. herman kapufi . amepiga marufu kwa Walimu Wakuu wa shule za Sekondari na Msingi wilayani humo  ambao wanajihusisha na upokeaji wafedha kutoka kwa wanafunzi kama michango na kwamba watakao bainika watachukuliwa hatua.

 Shule hiyo mpya ambayo imejengwa kwa nguvu za wananchi pamoja na fedha kutoka serikalini bado haijafunguliwa kutokana  na baadhi ya miundombinu vikiwemo vyoo kutokamlika licha ya kuandikisha wanafunzi wa darasa la kwanza.

No comments:

Post a Comment