Thursday 18 January 2018

DHANA YA UNYANYAPAA KWA WANAFUNZI WENYE ULEMAVU YAWA KIKWAZO KWAO

DSC_0254
Wanafunzi wenye mahitaji maalumu wakiwa darasani kwenye shule ya Msingi Mbugani Mjini Geita.

DSC_0281
Ubao wa shule ya msingi Mbugani kama unavyoonekana.

DSC_0283
Sehemu ya madarasa ya shule ya Msingi Mbugani.

Na,Joel Maduka,Geita

Licha ya jitihada za kuhakikisha watoto wenye ulemavu wanapata Elimu bora lakini bado baadhi ya wazazi na walezi wanaendelea kuwaficha watoto hao ili wasipate Elimu.

Mwalimu wa Elimu Maalum katika Shule ya Msingi Mbugani mjini Geita Bi Adella Buhabi  amefafanua kuwa bado kunatatiza kubwa kwa jamii ya kutokujitambua   na kujua thamani ya watoto hao hali inayosababisha baadhi ya wazazi na walezi kuwaficha.

“Tumeendelea na jitihada kadha wa kadha ya kuwatafuta watoto hawa na kuwaleta shuleni lakini changamoto kubwa ambayo tunakutana nayo ni kwa wazazi na walenzi kutokuwa tayari kuwaleta watoto hawa kupata masomo na wengine wamekuwa wakituuliza kama kuna hosteli au imekamilika ambayo inajengwa ili waweze kuwaleta  hali hii imekuwa ikiwadumaza sanaa watoto wengi” Alisema Mwl Buhabi.

Pamoja na hayo Mwl Buhabi  ameendelea kusisitiza kuwa wanafunzi wenye ulemavu wakiwezeshwa wanaweza kufanya vizuri zaidi ya wengine wasio na ulemavu.

Mmoja wa wanafunzi wenye ulemavu katika shule hiyo, Neema Mtesingwa alisema amekuwa anakerwa na kitendo cha baadhi ya watu kwenye jamii kuwanyanyapaa na kuwaona kama hawawezi kupata Elimu itakayowasaidia maishani mwao.

Utafiti uliofanywa na wataalam wa kimataifa wanaohudumia walemavu wa aina tofauti nchini ulibaini kuwa asilimia 98 ya makundi ya watoto wenye ulemavu hawapelekwi shuleni kwasababu mbalimbali ikiwemo dhana pototu katika jamii.

No comments:

Post a Comment