Friday 19 January 2018

MGODI WA GGM WAKABIDHI MRADI WA VIJANA NA WANAWAKE WENYE THAMANI YA BILIONI 2

DSC_0363
Jengo ambalo limekuwa likitumika kufundishia baadhi ya vikundi shughuli ya ushonaji kwenye mradi wa vijana na wanawake uliopo kwenye mtaa wa magogo kata ya Bomba mbili Wilayani Geita.

DSC_0239
Baadhi ya madawati ambayo yanatengenezwa kwenye karakana hiyo ya mafunzo  iliyopo kwenye mtaa wa magogo kata ya Bomba mbili iliyokuwa ikifadhiliwa na mgodi wa dhahabu wa Geita (GGM)Kabla ya kukabidhiwa kwenye mikono ya serikali ya Mkoa wa Geita.

DSC_0248

DSC_0260

DSC_0264
Meneja Mahusiano wa Mgodi wa GGM Manase Ndoroma akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya mradi wa vijana na wanawake.

DSC_0275
Mkurugenzi Mtendaji wa GGM Richard Jordinson akisisitiza mgodi huo kuendelea kutoa ushirikiano katika miradi mbali mbali ya kiuchumi na ya kimaendeleo Mkoani Geita.

DSC_0289
Meneja mahusiano wa mgodi wa dhahabu wa Geita(GGM)Manase Ndoroma akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita ,Mhandisi Robert Luhumbi baada ya kutembelea kwenye moja kati ya darasa la ufundi wa ushonaji.

DSC_0313
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akikagua baadhi ya mashine za kushonea nguo kwenye mradi wa vijana na wanawake ambao kwasasa umekabidhiwa kwenye mikono ya serikali ya halmashauri ya mji wa Geita.

DSC_0357
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akizungumza na wananchi ambao walipata nafasi ya kushuhudia makabadhiano hayo ambayo yalifanyika katika maeneo uliopo mradi huo.
DSC_0347
Baadhi ya wananchi wakiwa kweneye shughuli ya makabidhiano .

Na,Joel Maduka ,Geita.

Mgodi wa dhahabu wa Geita, GGM umekabidhi mradi wa kuwawezesha vijana na wanaweke kujikwamua kiuchumi wenye thamani ya zaidi ya Sh Bilioni 2 kwenye halmashauri ya mji wa Geita.

Mradi huo unahusisha shughuli za uchomeleaji wa vyuma, ushonaji wa nguo, utengenezaji wa viatu na ufyatuaji wa matofali ya kisasa.

Hatua hiyo imefuatia uamuzi wa serikali mkoani Geita kutaka ikabidhiwe majengo ya mradi huo yaliyojengwa kwa ufadhili wa mgodi wa GGM yaliyopo Mtaa wa Magogo yabadilishwe kuwa Chuo cha Ufundi, VETA kwa lengo la kuwasaidia vijana wengi zaidi kupata ujuzi wa ufundi Mkoani humo.

Akizungumza katika makabidhiano ya mradi huo Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel amesema atahakikisha taratibu za kuwa chuo zinakamilika kwa muda mfupi huku akiagiza Halmashauri ya Mji wa Geita kusimamia kikamilifu jambo hilo.

Mmoja wa wajasiriamali walio katika mradi huo Bw Isack Mabula amesema tangu wawekwe kwenye mradi huo hawajafanikiwa kujiendeleza kutokana na mgodi kugoma kuendelea kuwafadhili.

Aidha Mkuu wa Mkoa wa Geita ametoa onyo kwa wote wanaohujumu miradi ya maendeleo ya wananchi.

Manase Ndoroma ni Meneja Mahusiano wa Mgodi wa GGM amesema mategemeo yao ni kuona mradi huo ukiendelezwa na serikali na kwamba Utawanufaisha wananchi wengi zaidi hususani vijana na wanawake.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita Mhandisi Modest Apolinary amesema mradi huo utatoa fursa nyingi za kuwawezesha walengwa kujifunza na hatimaye kujitegemea katika shughuli za kiuchumi

No comments:

Post a Comment