Wednesday 31 January 2018

WANANCHI GEITA WAOMBA ELIMU ITOLEWE ZAIDI JUU YA MFUMO MPYA WA TEHAMA

DSC_1403
Watumishi wa mahakama Wilaya ya Geita wakiwa kwenye ufunguzi wa wiki ya sheria na hapa wakimsikiliza mkuu wa Wilaya ya Geita.Mwl Herman Kapufi.

DSC_1388
Mkuu wa wilaya ya Geita.Mwl Herman Kapufi akisisitiza wananchi kujenga desturi ya kujua sheria na kujifunza mambo mbali mbali ambayo yanahusu sheria wakati wa uzinduzi wa wiki ya sheria Wilaya humo.


DSC_1419
Mtendaji wa mahakama ya wilaya ya Geita,Bw Lothan Simkoko akimshukuru Mkuu wa wilaya kuzindua wiki ya sheria .

DSC_1430
Wanafunzi wa shule ya msingi Kalangalala wakiimba wimbo wenye maudhui ya  siku  ya sheria .


Na,Joel Maduka,Geita.


Wananchi Mkoani Geita Wameiomba Mahakama kutoa mafunzo ya kutosha kuhusu mfumo mpya wa TEHAMA unaotarajiwa kuanza kutumika kwenye kesi mbalimbali.

Mfumo wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano unatajwa kuwa utaongeza ufanisi kwenye mahakama kwa maana ya kutoa fursa kwa mwananchi aliye nje ya nchi kutoa ushahidi kwenye mahakama zilizopo nchini.

Mfumo unaweza kuwa ni mzuri lakini tatizo ni elimu ni wananchi wangapi wanaelimu na mambo ya teknolojia kwanza tukiangalia kuna baadhi yao ni waoga hata kufika kwenye mahakama leo hii unadhani wataujua mfumo huo mimi naomba mahakama itoe elimu zaidi na sio kusubilia hadi siku ya Mahakam ndio watoe elimu” Alisema Kimamba Amiri mkazi wa mjini Geita.

“Kuhusu teknolojia ambayo inazinduliwa na mahakama itatusaidia kwendana na wakati mimi nafikili sasa nchi yetu inakwenda na mambo ya teknolojia kitu ninachokiomba kwenye mahakama ni kuondokana na vitendo vya unyanyasaji kwenye maeneo ya mahakamani” Alisema John Matiba.

Hata hivyo  Kaimu Hakimu Mkazi mfawidhi mahakama ya Mkoa  wa Geita, Ushindi Swalo ambaye alisema lengo ni kuondokana na mfumo wa zamani wa kutumia karatasi nyingi na kwamba utaratibu huo utasaidia kuonesha kesi nyingi kwa urahisi zaidi hata kwa mtu aliyembali kuona kesi yake kama inaendelea kwenye tarehe husika au imehairishwa.

Aidha mkuu wa wilaya ya Geita Mwl Herma Kapufi amewataka wananchi kujitahidi kujua sheria kwa kuwa mambo mengi yanaendeshwa kwa misingi ya sheria.

No comments:

Post a Comment