Thursday 18 January 2018

GUMU WA MAISHA WASABABISHA WANAFUNZI WA KIKE KUTOKUMALIZA MASOMO WILAYANI NYANG'HWALE

WANAFUNZ%2B2
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Msalala wakiwa kwenye mazingira ya shule hiyo.

WANAFUNZ
Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Msalala wakitoka shule kuelekea Nyumbani wakitumia usafiri wa Baiskeli.

DC%2BGWEYAMA
Mkuu wa Wilaya ya Nyang’wale Mkoani Geita , Bw Hamim Gweyama akielezea mikakati ya kuendelea kuwalinda watoto wa kike dhidi ya mimba za utotoni. 


Na Joel Maduka, Nyang’wale.

Ugumu wa maisha katika baadhi ya familia Wilayani Nyang’hwale Mkoani Geita umetajwa kuwa moja ya sababu za wanafunzi wa kike wa sekondari kurubuniwa na wanaume kwa kuwapa fedha na hivyo kupata mimba za utotoni.

Takwimu za mimba kwa wanafunzi wa kike kwa shule za sekondari na msingi wilayani humo katika kipindi cha mwezi January hadi Disemba mwaka jana zilikuwa mimba 52 na kati ya hizo wanafunzi wa Sekondari ni 37 na wa shule ya msingi ni 15 na kwamba wote walipoteza sifa za kuendelea na masomo.

Mkuu wa Wilaya hiyo Bw Hamim Gweyama amesema miongoni mwa mikakati 10 walionayo kwa mwaka huu kupambana na tatizo la mimba mashuleni.

Hata hivyo katika mimba hizo 52, hakuna kesi hata moja iliyohukumiwa hadi sasa lakini ziko kwenye hatua tofauti, na kesi 45 ziko polisi na upelelezi bado unaendelea kufanyika na 7 ziko mahakamani ambapo mkuu wa wilaya hiyo amesema wana mikakati mingi ya kuwalinda watoto wa kike.

Mimba kwa wanafunzi zimetajwa kuongoza katika shule ya Sekondari ya Msalala ambapo mtandao huu umezungumza na Mkuu wa shule Bw ,David Mayega alisema kuanzia mwaka 2016 hadi 2017 katika shule hiyo kumekuwepo na mimba zaidi ya kumi na kitu na sababu kubwa ni umbali ambao wanafunzi wa kike wamekuwa wakitembea kwaajili ya kufuata Elimu.

Aisha Said ni mwanafunzi wa shule hiyo alisema kuwa muda mwingine wamekuwa wakifika nyumbani wanakuta hakuna chakula hali ambayo imekuwa ikipelekea walio wengi kuingia kwenye vitendo vya ushawishi na kurubuniwa na tamaa ya vitu vidogo.
 Hata hivyo wilaya ya Nyang’wale impokea Sh Milioni 150 kutoka Serikali kuu kwa ajili ya ujenzi wa mabweni ambapo tayari vifaa vimeanza kununuliwa na wakandarasi wanatafutwa kwa ajili ya kuanza ujeni huo.

No comments:

Post a Comment