Na, Joel Maduka, Geita
Wakazi wa Wilaya ya Chato Mkoani
Geita,wameiomba serikali kutekeleza kwa haraka miradi ya maji iliyoahidiwa kwa
muda mrefu kutokana na watu wengi kupata shida ya kutembea umbali mrefu
kutafuta maji
Baadhi ya wananchi hao Bi Anastazia Mashauri ambaye ni mkazi wa Kata ya
Ilemela na Bahati Mashauri ambaye ni mkazi wa Kata ya Muungano wameelezea kuwa
pamoja na jitihada ambazo serikali imeendelea kuzifanya kuwapatia maji lakini
hali bado mbaya kwani wengi wao hawapati maji safi na salama.
"Hali ya upatikanaji maji kijijini kwetu
ni mbaya sana kwani tunakisima kimoja tu hali ambayo imekuwa ikisababisha wengi
wetu kuelekea ziwani kutafuta maji na maji ambayo tunachota ya ziwani yanakuwa
sio masafi ila inaturadhimu kuchota tu kutokana na shida ya maji tunyopata hapa
kijijini kwetu tunaomba serikali itusaidia kiukweli tunapata shida sana" Alisema Bi Annastazia Mashauri.
Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo Bw Bathoromeo
Manunga amesema wanatarajia kutekeleza Miradi mikubwa miwili ya maji ambayo
itawanufaisha Wakazi elfu 62 ambapo kwa sasa ni asilimia 42 ya wakazi wanaopata
maji na salama.
Ameongeza kuwa mradi mmoja kati ya hiyo unategemea kuchukua maji kutoka
ziwa Victoria ambao utasambaza maji katika maeneo mbalimbali Wilayani Chato.
Mbunge wa Jimbo hilo Dr Medard Kalemani amewaambia Wananchi wa Ilemela,
Nyamboge na Kanyama kuwa awali walileta mradi wa visima vya kina kirefu lakini
bahati mbaya Mkandarasi alipokuja ilikua kipindi cha ukame na maji hayakutoka
na January 7 2018 Mkandarasi anakuja kupima tena.
No comments:
Post a Comment