Thursday 11 January 2018

CHAMA CHA CCM GEITA CHATOA SIKU 7 KWA JESHI LA ZIMA MOTO KUOMBA RADHI



Mjumbe wa  halmashauri kuu ya Taifa(NEC)  Iddi  Kassim Iddi akizungumza na wajumbe wa kikao cha halmashauri kuu ya mkoa ya chama hicho kwenye ukumbi wa halmashauri ya mji wa Geita.


Kamanda wa Jeshi la Zima Moto na uokoaji mkoani Geita Bw Elisa Mugisha akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni wakati alipokuwa akitoa taarifa ya shughuli ambazo wamezifanya kwa mwaka ambao umemalizika.

Chama cha mapinduzi Mkoani Geita kimelitaka jeshi la zima moto na uokoaji  Kuomba  radhi ndani ya siku saba kutokana na tuhuma ambazo zilielekezwa kwa viongozi wa chama hicho kuingilia kazi na utendaji wa jeshi hilo.

Hayo yamesemwa na Mjumbe wa  halmashauri kuu ya Taifa(NEC)  Iddi  Kassim Iddi,wakati alipokuwa kwenye  kikao cha halmashauri kuu ya mkoa ya chama hicho,alisema wao kama chama wamepokea kwa masikitiko makubwa tuhuma hizo ambazo zimeelekezwa kwenye chama hicho na  lengo lilikuwa sio kuingilia majukumu ya jeshi hilo ila ni kuwatetea wananchi wa Rwamgasa ambao walikuwa  wakiuziwa mitungi kwa bei kubwa  bila ya kupatiwa risti ya serikali.


“Watambue ya kuwa sisi chama na serikali ni kama baba na mwana  ni kwamba ni lazima kuhakikisha kwamba tunafanya kazi kwa pamoja na napenda kukanisha kuwa sisi hatuna uadui wala na jeshi la zima moto na tunampa siku saba akiombe radhi chama na viongozi wake kwani namna ambavyo amefanya ni kuchafuana”Alisema Kassim.

Aidha  Katibu mwenezi wa chama hicho Mkoani  humo,Devid Azaria ,amekanusha juu ya tuhuma  za viongozi wa chama kuingilia zoezi lao  na kwamba wanachokikataza  ni taratibu ambazo zilitumika za uuzwaji wa vifaa vya kuzimia moto kuwa zilikuwa za kuwalazimisha wachimbaji bila ya kuwapa elimu  jambo ambalo sio sahihi.

Hata hivyo mwenyekiti wa chama hicho Mkoani Humo.Alhaji Saidi Karidushi amewataka viongozi wote kufanya kazi kwa kutimiza majukumu yao na kwamba kama kuna tatizo ni vyema wakayashughulikia wao bila ya kutegemea nguvu kutoka kwake.


Kwa upande wake Kamanda wa Jeshi la Zima Moto na uokoaji mkoani Geita Bw Elisa Mugisha alipopigiwa simu na mtandao huu amekiomba radhi chama cha Mapinduzi huku akisisitiza kuwa baadhi ya viongozi wanaomiliki makarasha kulipia tozo zinazotakiwa na jeshi la zima moto ili kuepusha mtafaruku baina ya pande hizo mbili.




No comments:

Post a Comment