Mheshimiwa Kangi Lugola ,akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Geita Mwl Herman Kapufi na baadhi ya wananchi ambao wameathirika kutokana na maji Hayo kwenye maeneo ya mashamba.
Ekari 270 za mashamba ya wakulima
kwenye kijiji cha Ziwani Kata ya Nyarugusu Wilayani Geita zimeathiriwa na Sumu
iliyotoka kwenye Bwawa la kuhifadhia Kemikali lililopasuka kingo zake na maji
kusambaa kwenye mashamba hayo.
Hali hiyo imemlazimu Naibu Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Bw Kangi Lugola kuitaka
kampuni ya Madini ya Nyarugusu inayohusika na suala hilo kuwalipa fidia
wananchi 57 ambao mazao yao yameathirika.
Awali Bw Lugola aliagiza muwekezaji
huyo akamatwe kutokana na kile alichodai kuwa ni uvunjifu wa sheria za utunzaji
wa mazingira mgodini hapo na kwamba uongozi wa mgodi huo ulimzuia Afisa
Mazingira wa Wilaya ya Geita Bi Hellen Eustace kutekeleza majukumu yake baada
ya kufika mgodini hapo kukagua namna wanavyozingatia utunzaji mazingira
Bw Kangi alisema Mwekezaji haruhusiwi
kuendelea na shughuli anazozifanya na kufunga mgodi huo hadi watakapotekeleza
mambo waliyoelekezwa
Mkurugenzi wa Nyarugusu Mine Company
Bw Fred Masanja amesema kusimamishwa kwa shughuli zao kunaweza kuathiri
ytendaji wao kwa kuwa Tani Laki moja na 20 hawataweza kuzizalisha na hivyo
watapata hasara ya zaidi ya Sh Milioni 600 hadi 700
No comments:
Post a Comment