Katibu Mkuu wa Chama
cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana amesema yuko tayari kuendelea
kukitumikia chama hicho.
“Neno la mwenyekiti kwangu ni amri
kama umeona bado unahitaji niendelee kukusaidia niko tayari kufanya hivyo,”
alisema Kinana leo Jumatatu Desemba 18,2017 katika mkutano mkuu wa CCM
unaoendelea mjini Dodoma.
Kinana ametoa kauli
hiyo wakati kukiwa na minong’ono kuwa ameandika barua akiomba kuachia nafasi
yake ya ukatibu mkuu.
Awali, Mwenyekiti wa
CCM, Rais John Magufuli aliweka wazi kuwa Kinana amekuwa msaada mkubwa katika
kukiongoza chama hicho.
“Mzee Kinana
amenisaidia sana. Amenisaidia mno kwenye kufanya mabadiliko ndani ya chama na
ni mategemeo yangu ataendelea kunisaidia,” alisema.
Katika hatua nyingine,
Kinana ametoa siri ya ushindi wa kishindo wa chama hicho katika uchaguzi kuwa
ni kutokana na ilani bora, demokrasia na kusikilia maoni ya wanachama.
Kinana amesema
demokrasia imekuwa msingi wa chama hicho ndiyo sababu kinaimarika.
“CCM tunazingatia
demokrasia, wanachama wapo huru kutoa maoni ndani ya chama. Hili linafanyika
kwa kuwa usipowapa uhuru wa kusema ndani watasema nje,” alisema.
No comments:
Post a Comment