Monday 18 December 2017

SERIKALI MKOANI GEITA YAJIPANGA KUTATUA TATIZO LA MAJI KWA WANANCHI

DSC_0761
Mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Gabriel akiwa na Mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mjini Geita(GEUWASA)Mhandisi Joseph Mwita wakati alipotembelea moja kati ya mitambo ya kuzalishia maji ambayo hipo kijiji cha Nungwe kwenye ziwa viktoria.

DSC_0754
Eneo la mitambo ya uzalishaji wa maji ambayo hipo kijiji cha Nungwe.

DSC_0814
Fundi  wa mitambo ya maji kutoka mgodi wa dhahabu wa Geita,(GGM)Denis Domician akitoa maelezi namna ambavyo maji yamekuwa yakitibiwa kabla ya kusambazwa kwa watumiaji mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Geita.

DSC_0837
Fundi  wa mitambo ya maji kutoka mgodi wa dhahabu wa Geita,(GGM)Denis Domician  akitoa maelezo namna ambavyo maji yamekuwa yakipita na kutibiwa kwenye sehemu ambazo zimetengwa.

DSC_0846
Eneo la kutibia maji.

DSC_0862
Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshugulikia masuala ya Bonde la Ziwa Victoria Dr Ali Said Matano akielezea namna ambavyo jumuiya hiyo imeweza kuongeza muda kwa miradi ambayo ijamalizika hadi kufikia mwezi wa tisa mwakanai iwe imekamilika wakati wa ziara ya kutembelea vyanzo vya maji ambavyo vipo kwenye halmashauri ya mji wa Geita. 

DSC_0881
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Gabriel pamoja mhandisi wa maji wa Geuwasa wakitoa maelezo ya namna ambavyo Tanki hilo limekuwa kikifanya kazi wakati alipotembelea kwenye tanki hilo.

DSC_0890
Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Geita,Mhandisi Modest Aporinal akitoa maelezo ya namna ambavyo wanatarajia kupitisha mabomba kwenye mtaa wa 14 kambarage kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita.
Serikali mkoani Geita imejipanga kutatua kero ya maji kwa wananchi inayowakabili wananchi kwa muda mrefu.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel ametoa kauli hiyo alipotembelea miradi ya uzalishaji wa maji inayosimamiwa na Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira jinni Geita, GEUWASA.

Alisema serikali imedhamiria kuona mji wa Geita unakuwa na maji ya kutosha ambapo kwa sasa kuna tanki lenye Mita za ujazo elfu moja na mia mbili  na kwamba zipo jitihada za kuweka pampu itakayosaidia kuongeza maji kwenye tanki hilo ili kuweza kuongeza zaidi uzalishaji wa maji kwa maeneo ya mji huo.

Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshugulikia masuala ya Bonde la Ziwa Victoria Dr Ali Said Matano alisema mji wa Geita utanufaika na awamu ya tatu ya mradi wa maji kutoka Ziwa hilo kwa ufadhili wa Benki ya Afrika.

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira mjini Geita, GEUWASA Bw Joseph Mwita amesema mahitaji ya maji mjini Geita ni Mita za ujazo  15 160 na kwamba maji yanayozalishwa ni Mita za ujazo kati ya  3 500 hadi 4000.

No comments:

Post a Comment