Kahimu
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita akielezea juu ya utatuzi wa tatizo
ambalo limeonekana kwenye kijiji hicho juu ya kuuzwa kwa eneo ambalo lilikuwa
limetengwa kwaajili ya matumizi ya stendi.
Mbunge wa
Jimbo la Geita Vijijini,Joseph Msukuma akizungumza na wanakijiji wa kijiji cha
Ihanamilo Kata ya Nkome wakati za zoezi la kuondoa Vigingi ambavyo viliwekwa
kwenye eneo ambalo limetengwa kwaajili ya ujenzi wa Stendi ya mabasi kijijini
Hapo.
Wananchi
wakifuatilia mkutano.
Mbunge wa Jimbo la Geita
Vijijini Mh,Joseph Kasheku Msukuma ambaye pia ni mwenyekiti wa
chama cha mapinduzi CCM Mkoani Geita ameongoza mamia ya wananchi wa kijiji cha ihanamilo Kata ya Nkome Wilayani Geita kutoa visiki ambavyo viliwekwa na mtu
ambaye inasadikika amenunua eneo la kijiji linalokadiliwa kuwa ni
hekari moja na nusu ambalo lilitengwa kwa matumizi ya stendi kutoka kwa
serikali ya kijiji.
Hatua hiyo imekuja
baada ya Serikali ya Kijiji ikiongozwa na Mwenyekiti wa Kijiji hicho ,Bw Thomas
Alila na mtendaji wa kijiji Charles Mbilingi kuuza eneo kwa kiasi cha sh
,Milioni sita (6).
Kwa maelezo ya afisa
mtendaji wa Kijiji Charles Mbilingi amesema kuwa tarehe 15 mwezi huu walikaa
kwenye kikao na wanakijiji na kuamua kwamba wauze eneo hilo ili liweze
kusaidia ujenzi wa shule.
“Tulikaa kama halmashauri
ya Kijiji tukajadili namna ya kutatua changamoto ya kukosekana kwa shule kwenye
kijiji chetu tulipojadili tukaonelea kwa sababu tuna eneo ni bora tuliuze ili
tuweze kupata pesa ambazo zitasaidia ujenzi wa madarasa na hatukufanya peke
yetu
tuliwashirikisha wananchi
wa kjiji wakawa wamekubali”Alisema Mtendaji.
Hata Hivyo kutokana na
maelezo hayo ya mtendaji wa Kijiji Mbunge Msukuma amewaeleza wananchi
ambao walikuwa kwenye Mkutano wa hadhara kuwa eneo hilo liliuzwa tarehe tano
mwezi huu jambo ambalo yeye alilikataa kutokana na faida ambazo zinaweza
kupatikana kutokana na uwepo wa eneo hilo.
“Nimesikitishwa sana na
kitendo ambacho kimefanyika cha kuuzwa eneo hilo kiasi cha Shilingi milioni
sita (6) na mimi nilimpigia simu mtendaji nikamwambia azirudishe pesa
aende halmashauri kuna maelekezo kwa mkurugenzi na tutambue kuna maeneo muhimu
lazima yawepo leo(jana)ninakwenda kung’oa visiki vyote”Alisema Msukuma
Katika hali isiyo ya
kawaida Diwani wa Kata ya Nkome Masumbuko Nsembe amejikuta jina lake
likiwa limeandikwa kuwa ni miongoni kati ya viongozi ambao walilidhia
kuuzwa kwa eneo la kijiji.
“Mheshimiwa Mbunge mimi
sikuuza nilifika saa kumi na moja nilikuta wakisoma hiyo taarifa ya kuuza
lakini mimi niliwaambia kuwa wasiuze eneo hilo kwa hicho kiasi.”Alisema Diwani
Katika hali isiyo ya
kawaida wananchi ambao walihudhuria kikao hicho cha kukubaliana kuuzwa
kwa eneo hilo walipotajwa majina yao walijikuta wakidai kushindwa kujua
hali hiyo imetokana na nini na kama waliingizwa mkenge kwenye mauziano hayo.
Kutokana na hatua ambayo
mbunge ameifanya ya kuongeza wananchi kutoa visiki wananchi wameshukuru na
kusema kuwa walikuwa hawajui kama eneo lao limeuzwa.
No comments:
Post a Comment