Kufuatia agizo la Waziri wa Fedha na Mipango,Dk
Philip Mpango la kuzitaka mamlaka za mapato Nchini (TRA)kufanya ukaguzi nchi
nzima ili kubaini wamiliki wa vituo vya
mafuta wanaokiuka maagizo ya serikali yaliyowataka wafunge mashine maalum za
kielektroniki za kutolea risiti(EFD)tangu mwaka jana.
Baadhi ya watumiaji wa Huduma ya Mafuta Wilaya na Mkoa wa Geita,Bi Julian Kimaro na Halfan Rajabu ,wamesema
kukosekana kwa Huduma hiyo wameathirika
kwa kiasi kikubwa kwani tangu siku ya
jana majira ya jioni na alfajiri ya saa
kumi wamekuwa kwenye foleni wakisubiri kupata mafuta na kwamba ni Kituo kimoja tu ndicho ambacho kinatoa
huduma hiyo.
Baadhi ya Mameneja wa vituo vya mafuta Moil na Tropical ,James Zabron na Ismail Adam,wamesema
kuwa wameenda Kwenye mamlaka ya mapato kununua mashine hizo lakini hawajazipata
kwa madai kuwa hata TRA pia hawana mashine hizo na tatizo lipo kwa mafundi wa
kufunga kwenye injini za mafuta.
Mwenyekiti wa chama cha wamiliki na waendeshaji wa vituo
vya mafuta(TAPSOA) mkoani Geita, Hamis Tabasamu
amesema kuwa tatizo ni bei ya mashine
hali ambayo imewafanya wafanyabiashara walio wengi kushindwa kununua mashine
hizo.
Meneja wa TRA Mkoani Geita,Samuel Nkonya amesema
kuwa zoezi ambalo linaendelea ni la
kufanya ukaguzi kwenye vituo vyote lengo likiwa ni wamiliki kuwa na mashine za
kutoa risiti ambazo zinafungwa kwenye Mtambo wa utoaji wa mafuta na kwamba jumla ya vituo 18 hadi sasa vimefungwa na
kituo ambacho kinafanya kazi ni kimoja tu.
Zoezi la kufunga vituo vya mafuta ambavyo havina
mashine za EFD ni la nchi nzima
No comments:
Post a Comment