Baadhi ya wananchi wakiwa kwenye Kisima cha maji ambacho kimejengwa na
mgodi wa Nyamutondo kwenye Kata ya Kaseme Wilayani Geita.
Mkuu wa Wilaya ya Geita Mwl Herman Kapufi akikagua moja kati ya visima
ambavyo aliagiza vijengwe kwenye Kijiji Nyamutondo na mwekezaji ambaye ni
mchimbaji mdogo.
Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akimuuliza moja kati ya
wananchi wa Kijiji hicho Bi, Koku Gerevasi,kama amelizishwa na
visima ambavyo vimetengenezwa na Mgodi wa Nyamutondo.
Mkurugenzi wa Mgodi wa dhahabu wa Nyamutondo Bw.Martin Benda
Kajoro,akikabidhi visima hivyo Kwa Mkuu wa Wilaya ya Geita na Kuomba radhi
kutokana na kushindwa kutekeleza agizo lake la mara ya kwanza.
Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akizungumza na wananchi na
kutoa maelekezo ya kutunza visima ambavyo vimejengwa kwa gharama kubwa.
Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akikata utepe ishara ya
kuzindua visima hivyo.
Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi,akimtwika ndoo ya maji baada ya
kuzindua visima hivyo
Serikali wilaya ya Geita kufikisha nishati ya Umeme katika Kitongoji cha Nyamutondo kijiji na kata ya Kaseme kabla ya Mwezi Oktoba mwaka huu ili kuwezesha Pampu za visima vya maji kutumia Umeme na kusambaza maji kuwafikia wananchi kwa urahisi zaidi.
Hatua hiyo ya Serikali imekuja ni baada ya
Kukamilika kwa Ujenzi wa Visima viwili kati ya vinne ambavyo vimechimbwa na
wawekezaji wa mgodi wa dhahahu wa Nyamutondo uliopo Kijiji hicho ambavyo
vimejengwa kwa gharama ya shilingi Milioni hamsini na nne (54).
Akizindua visima hivyo na Kukabidhi kwa serikali ya
Kijiji Mwl.Herman Kapufi ,amesema uwezo wa kusukuma maji kwa sasa
katika visima hivyo ni mdogo kutokana na pampu ambazo wananchi wanazitumia kwa
mikono na kwamba kupatikana kwa nishati ya umeme kutarahisisha na kuboresha
huduma ya maji
“Kazi yangu ni kuhakikisha umeme unaletwa hapa ili
kurahisisha swala la maji na kufikia mwezi wa Kumi umeme utakuwa umefika kwenye
kijiji hiki”Alisema Kapufi.
Naye Mkurugenzi wa Mgodi wa dhahabu wa Nyamutondo
Bw.Martin Benda Kajoro amesema kukamilika na kuzinduliwa kwa visima hivyo
kutaondoa changamoto ya maji kwa wananchi iliyopelekea kufungwa kwa shughuli za
uchimbaji wa dhahabu kushinikiza wawekezaji kuchimba
visima.
“Kweli kulikuwa na shida kubwa sana ya maji lakini
kutokana na hali hiyo Mkuu wa wilaya alituagiza kujenga visima virefu vya maji
na sisi tulitilia maanani agizo lake na ndio maana leo (jana) tumemaliza na
tumekabidhi kwake hivyo tunamwomba tu afikishe kwa afisa madini aweze
kutufungulia mgodi wetu maana kwa sasa hatufanyi shughuli zozote”Alisema Kajoro
Baadhi ya wananchi wa kijiji hicho ambao
wamezungumza na mtandao wa maduka online ,Semeni John na Koku
Gerevasi wamesema walikuwa wakikabiliana na changamoto ya kukaa
kwenye foleni kwa muda mrefu na wakati mwingine kujikuta wakikabiliana na
vurugu.
No comments:
Post a Comment