Thursday 21 September 2017

TRA NA TCCIA YAWAKUTANISHA NA KUWAPA ELIMU YA KULIPA KODI WAJASIRIAMALI WADOGO MKOANI GEITA





 Baadhi ya vikundi vya wajasiriamali wakifuatilia Semina ambayo ilikuwa inafanyika katika ukumbi wa halmashauri ya Mji wa Geita.


 Kikundi cha wasaniii ambacho kinajihusisha na shughuli za ujasiriamali  kikifuatilia semina.          

Chama cha wafanyabiashara wenye viwanda na wakulima TCCIA Mkoani Geita kwa kushirikiana na mamlaka ya mapato Nchini (TRA) imewakutanisha wafanyabiashara wadogo na wakubwa kwa lengo la kuwapatia elimu  ambayo itawasaidia  kulipa kodi.
Akizungumza na wafanyabiashara hao ambao walikuwa wamejitokeza kwenye ukumbi wa halmashauri ya Mji wa Geita,Mgeni Rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya  Geite ,Mwl Herman Kapufi ,amesema wajasiriamali wanatakiwa kusajiliwa na kujua elimu ya mlipa kodi ambayo itawasaidia kujulikana  na kutambulika  serikalini. 

Akizungumza na Stormfm Meneja wa TRA Mkoani Geita, James Jilala amesema kwa mujibu  wa mabadiliko  ya sheria  za nchi  wafanyabiashara ambao wanakuwa sio rasmi wanatakiwa kuwa kwenye vikundi maalum ambavyo vitatambuliwa na kupatiwa elimu ambayo itawasaidia kuwa walipa kodi wazuri.

Katibu  wa TCCIA Mkoani Humo,Mariam Mkaka ameelezea kukosekana elimu ya ujasiriamali ni chanzo ambacho kimekuwa kikisababisha vikundi vingi kutokusimama  na  kujikuta vinaanguka.

Baadhi  ya wafanyabiashara wadogo  ambao wameshiriki katika semina hiyo, Rose Michael ,Jackson Mlenga na Winfrida Marius wameeleza kuwa semina hiyo itawasaidia kupata Elimu ya ulipaji Kodi.

No comments:

Post a Comment