Saturday 23 September 2017

JUMUIYA YA UMOJA WA WANAWAKE, (UWT) WILAYA YA GEITA WAPATA MWENYEKITI MPYA


Mwenyekiti ambaye amechaguliwa kwenye Jumuiya ya wanawake wa chama cha mapinduzi Wilayani Geita Bi,Antonia Charles akiwashukuru wajumbe kwa kumchagua kukalia kiti uwenyekiti Ngazi ya Wilaya ya Geita  kwa muda wa miaka mitano


Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Geita Mahimuna Mingisi amesisitiza kuendelea kuwepo kwa mshikamano ndani ya Jumuiya Hiyo.

Msimamizi Msaidizi wa uchaguzi Ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akiwashukuru wajumbe kwa namna ambavyo wamejitokeza kufanikisha uchaguzi huo.


Wajumbe wakifuatilia Mkutano huo na uchaguzi.



Msimamizi Mkuu wa uchaguzi ambaye ni katibu wa Chama cha mapinduzi Wilaya ya Geita,Julius Peter akiwakilisha matokeo ya uchaguzi.

Katibu wa UWT Wilaya ya Geita,Mazoea Salum akifuatilia matokeo.

Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi, UWT Wilayani Geita imemchagua Bi Antonia Charles Kushika kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo.

Msimamizi mkuu wa uchaguzi huo, Katibu wa CCM wilayani humo Bw Julius Peter amesema kati ya kura 583 zilizopigwa, kura zilizoharibika ni 17 ambapo wagombea walikuwa Bi Amina Shaaban, Mariam Hamed na Antonia Charles.

Mwenyekiti mpya wa UWT Bi Antonia Charles ameahidi kuunda vikundi vitakavyowasaidia wanawake wa umoja huo kupata mikopo itakayowasaidia katika ujasiriamali.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa UWT anayemaliza muda wake Bi Khadija Said amemuomba mwenyekiti mpya kutekeleza majukumu ya Jumuiya hiyo kikamilifu.

No comments:

Post a Comment