Friday 22 September 2017

TCRA: BLOGU NA ONLINE TV ZITUMIKE KATIKA UJENZI WA TAIFA


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) Bw. James Kilaba (katikati) akiandika maoni ya wadau wa mitandao ya blogu na Online Tv wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kusisitiza matumizi bora ya mitandao ya kijamii kwa awamu ya pili mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Serikali ya Awamu ya Tano kupitia Mamlaka ya Mawasiliano nchini(TCRA) imetia nia kuboresha mawasiliano kwa umma hasa katika matumizi ya mitandao ya kijamii ili kuwawezesha watanzania kupata elimu bora ya maendeleo na kujenga uchumi uliobora.

Haya yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Bodi wa Mamlaka hiyo Dkt. Jonas Kilimbe  alipokua akihutubia hadhara ya wamiliki wa vyombo vya habari mtandaoni (blogu na Online TV) katika uzinduzi wa kampeni ya awamu ya pili ya “kusisitiza matumizi bora ya mitandao ya kijamii”  iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere.

Katika hafla hiyo, Dkt. Kilimbe alisema kuwa kwa sasa teknolojia ya mtandao inakua kwa kasi kwa hiyo huduma za habari zinapatikana kila sehemu kwa njia ya mtandao na kufanya matumizi ya mitandao kuwa makubwa.

“Sekta ya mawasiliano kwa umma imepiga hatua kubwa sana duniani kwa sasa, kwa kiasi kikubwa mtandao unachangia kuwepo kwa habari nyingi. Tanzania inajumla ya televisheni za mitadaoni zipatazo 50 pamoja na blogu 150 ambazo zote zinatoa taarifa kwa wananchi, hii inaashiria kuwa mawasiliano kwa umma yamehamia zaidi kwenye mtandao”, alisema Dkt.Kilimbe.

Aidha Dkt.Kilimbe alisema kuwa sekta hii inapaswa kuangaliwa zaidi kwani ni sekta muhimu kwa ujenzi wa Taifa na kuwaasa vijana kutumia vizuri teknolojia hiyo kwa kujielimisha kuhusiana na masuala ya maendeleo kuliko kutumia vibaya mitandao hiyo.

Tuna jukumu zito na ni kubwa kwa sababu sekta hii ya mawasiliano imeshikiria kila kitu na tasnia ya habari ina nguvu kubwa sana kwa kuleta elimu ya maendeleo kwa wananchi kwa hiyo waandishi mitandaoni tumieni weledi  mkubwa kwa habari za maendeleo.”, alisisitiza Dkt. Kilimbe.

Dkt.Kilimbe alisema kuwa katika matumizi ya teknolojia hii mpya yanapaswa kuzingatiwa  kwa ajili ya ujenzi wa taifa hasa kwa wale wanaotumia vizuri mitandao ya kijamii inawapa elimu kubwa ya maendeleo.

Aidha Dkt. Kilimbe amekishukuru chama cha wamiliki wa blogu na televisheni mtandaoni(TBN) kwa kuleta umoja na kuzingatia maadili na weledi wa umilikajia wa vyombo hivyo kwa kuwahabarisha wananchi.

Naye mtoa mada na mwakilishi kutoka TCRA Bw. Thadeus Lingo alisisitiza usalama wa matumizi ya mtandao akisema kuwa idadi ya watumiaji wa mitandao imeongezeka duniani kuanzia Julai 1, 2017 na kufikia bilioni 3.8 huku kati ya hao bilioni 3.4 ambayo ni sawa na asilimia 92 ni watumiajia wa mitandao ya kijamii hali iliyosababisha kuongezeka kwa vyombo vya habari kuhamia mtandaoni, kwa hiyo weledi unahitajika katika kuhabarisha umma kwa njia hii.

Kwa upande wake mratibu masaidizi wa polisi kitengo cha makosa ya kimtandao (Cybercrime) Bw.Joshua mwangasa alisema kuwa watumiaji wa mitandao ya kijami wanapaswa kutumia mitandao hiyo kwa makini zaidi ili kujiletea maendeleo na kuepusha matumizi ya lugha za matusi.

Akizungumzia sheria ya makosa ya kimtandao ya mwaka 2015 katika kifungu kidogo cha 16 kinachoelekeza kuchapisha habari za uongo mtandaoni kuwa ni uvunjaji wa sheria hiyo.

Mwangasa alisema kuwa kuanzia mwaka 2015 zaidi ya kesi 5172 ziliripotiwa huku mwaka 2016 kesi 7889 zilipelekwa mahakamani kwa kusikilizwa zaidi lakini mwaka 2017 kesi zilikuwa 3346 zimefikishwa mahakani na kituo cha polisi.

Aidha mwangasa ameeleza kuwa anga la mawasiliano kwa Tanzania liko salama kwa matumizi ya wanahabari na watanzania kwa ujumla.


Anga letu la cyberspace ni salama sana ukilinganisha na nchi zingine za ukanda wa maziwa makuu kwa hiyo tutumie fursa hii kwa kujiletea maendele na siyo kutumia kwa uharifu wa matusi na lugha zingine za kejeli”, alisema Bw,Mwangasa.

No comments:

Post a Comment