Friday, 8 June 2018

HOFU, KUTOJIAMINI ZAPELEKEA UPOTEVU WA HAKI KWA WANAWAKE GEITA


Baadhi ya wadau wa kupinga ukatili wa kijinsia kwa mwanamke wakiwa kwenye kikao cha pamoja kilichokuwa kimelenga kujadili sera na sheria ya ukatili dhidi ya Mwanamke kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa kanisa la Anglikana Mjini Geita.


Wadau wakisikiliza maelekezo kutoka kwa mwanasheria wa shirika lisilo la kiserikali la Woman promotion center.


Mwanasheria wa shirika lisilo la kiserikali la Woman Promotion Center ,Bi, Walta Caros akizungumza na waandishi wa habari juu ya sheria ya vitendo vya kikatili kwa mwanamke.

VYUO 20 VYAFUTIWA USAJILI NA BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)




Leo June 8, 2018 Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) limefuta usajili wa vyuo 20 kwa kushindwa kufuata utaratibu wa usajili wa vyuo vya ufundi na upungufu wa Rasilimali za kufundishia

MFUMUKO WA BEI NCHINI WAENDELEA KUPUNGUA TOKA 3.8% HADI 3.6%


Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ephraim Kwesigabo akifafanua jambo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu mfumko wa bei wa Taifa leo Jijini Dar es Salaam, Mfumuko wa bei umeshuka toka asilimia 3.8 mwezi Aprili hadi kufikia 3.6 Mei. Kushoto ni Meneja wa Ajira na Bei toka NBS, Ruth Minja. 

Thursday, 7 June 2018

PM MAJALIWA - TUNA KAZI KUBWA YA KUELIMISHA JAMII KUHUSU FISTULA


Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan amesema bado kuna kazi kubwa kuhakikisha jamii inafikishiwa ujumbe kuhusu tatizo la fistula na athari zake kwa afya ya mama na uchumi kwa ujumla.
Mama Samia amesema hayo leo Alhamisi Juni 7, alipozungumza katika Viwanja vya Hospitali ya CCBRT ambako alifanya ziara kujionea huduma mbalimbali zinazotolewa hospitalini hapo.

MKUU WA MAJESHI AHAMASISHA VIJANA KUJIUNGA NA JKT


Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi  Jenerali Venance Mabeyo amewahamasisha vijana kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa ili waweze kupata stadi za ufundi na hatimaye wajiajiri badala ya kutegemea kuajiriwa na Serikali.

Tuesday, 5 June 2018

MAKAMU WA RAIS ASHIRIKI KATIKA UZINDUZI WA UKUTA JIJINI DSM


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akisisitiza jambo kwa wananchi (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa ukuta wa ufukwe wa bahari uliojengwa kando ya barabara ya Barack Obama jijini Dar es Salaam, ukuta huo umejengwa kwa ufadhili wa mfuko wa Dunia wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi.


Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mhandisi Joseph Malongo akifafanua jambo kwa wananchi (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa ukuta wa ufukwe wa bahari uliojengwa kando ya barabara ya Barack Obama jijini Dar es Salaam, ukuta huo umejengwa kwa ufadhili wa mfuko wa Dunia wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi.


Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa, Alvaro Rodriguez akizungumza na wananchi (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa ukuta wa ufukwe wa bahari uliojengwa kando ya barabara ya Barack Obama jijini Dar es Salaam, ukuta huo umejengwa kwa ufadhili wa mfuko wa Dunia wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba, akifafanua jambo kwa wananchi (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa ukuta wa ufukwe wa bahari uliojengwa kando ya barabara ya Barack Obama jijini Dar es Salaam, ukuta huo umejengwa kwa ufadhili wa mfuko wa Dunia wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi.


Baadhi ya waandishi wa habari wakiendelea na majukumu yao wakati wa sherehe za uzinduzi wa ukuta wa ufukwe wa bahari uliojengwa kando ya barabara ya Barack Obama jijini Dar es Salaam, ukuta huo umejengwa kwa ufadhili wa mfuko wa Dunia wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akikagua ukuta wa ufukwe wa bahari uliojengwa kando ya barabara ya Barack Obama jijini Dar es Salaam mara baada ya kuuzindua mapema hii leo, ukuta huo umejengwa kwa ufadhili wa mfuko wa Dunia wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi.


Sehemu ya kupumzika iliyojengwa katika ukuta wa ufukwe wa bahari ya Hindi uliojengwa kando ya barabara ya Barack Obama jijini Dar es Salaam, ukuta huo umejengwa kwa ufadhili wa mfuko wa Dunia wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi.


Msanii Beka Fleva akitoa burudani kwa wananchi wakati wa sherehe za uzinduzi wa ukuta wa ufukwe wa bahari uliojengwa kando ya barabara ya Barack Obama jijini Dar es Salaam, ukuta huo umejengwa kwa ufadhili wa mfuko wa Dunia wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi.


Baadhi ya wananchi wakimsikiliza Makamu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan,(hayupo pichani) wakati wa sherehe za uzinduzi wa ukuta wa ufukwe wa bahari uliojengwa kando ya barabara ya Barack Obama jijini Dar es Salaam, ukuta huo umejengwa kwa ufadhili wa mfuko wa Dunia wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akiwapungia wananchi mara baada ya kuzindua ukuta wa ufukwe wa bahari uliojengwa kando ya barabara ya Barack Obama jijini Dar es Salaam, ukuta huo umejengwa kwa ufadhili wa mfuko wa Dunia wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi. Picha na Eliphace Marwa 

KINARA WA UTEKAJI AUWAWA MKOANI GEITA



Mtu mmoja anayejulikana kwa majina ya Panda Kinasa mwenye miaka 36 anayetuhumiwa kuwa kinara wa utekaji  watu ameuwawa kwa kupigwa na risasi makalioni wakati akijaribu kuwatoroka polisi baada ya kuwapeleka kwenye mashimo alikokuwa ametupa miili ya watu wawili wilayani Bukombe Mkoani Geita.