Mkuu wa Wilaya ya Geita Mwl. Herman Kapufi amewataka wanasheria kuwasaidia
wananchi kujua elimu ya sheria kutokana na wengi wao kushindwa kujua sheria
hali ambayo inasababisha wengi kukosa haki zao za msingi pindi wanapofuatilia
haki zao.
KUHABARISHA NA KUFAHAMISHA KUHUSU HABARI NA MAMBO YANAYOENDELEA KATIKA JAMII YA GEITA, KANDA YA ZIWA, TAIFA NA DUNIANI. TUTUMIE HABARI AU WASILIANA NASI KUPITIA info@stormfm.co.tz au +255 685 883 870
Tuesday, 30 May 2017
PICHA: YALIYOJIRI KIKAO CHA 37, MKUTANO WA 7 BUNGE LA 11 MJINI DODOMA LEO MAY 30, 2017

Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Najma Giga
akiongoza kikao cha 37 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leoMjini Dodoma Mei
30, 2017.

Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe akijibu
maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 37 cha Mkutano wa Saba wa Bunge
la 11 leo Mjini Dodoma Mei 30, 2017

Waziri Mkuu wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza jambo na Mbunge wa Kaliua(CUF)
Mhe.Magdalena Sakaya katika kikao cha 37 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo
Mjini Dodoma Mei 30, 2017.
Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akijibu maswali
mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 37 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11
leo Mjini Dodoma Mei 30, 2017.
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe.Angelina Kairuki akijibu maswali mbalimbali ya
wabunge katika kikao cha 37 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma
Mei 30, 2017.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Khamis
Kigwangalla akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 37 cha
Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leoMjini Dodoma Mei 30, 2017.
Naibu Waziri wa Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dk.Susan Kolimba akijibu maswali mbalimbali
ya wabunge katika kikao cha 37 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leoMjini
Dodoma Mei 30, 2017.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akijibu maswali
mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 37 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11
leoMjini Dodoma Mei 30, 2017.
Waziri wa Fedha na Mipango Dk.Philip Mpango akisoma Hotuba ya Makadirio ya
Mapato na Matumizi ya Wizara ya Fedha na Mipango kwa mwaka wa Fedha 2017/2018
katika kikao cha 37 cha Mkutanowa Saba wa Bunge la 11 leoMjini Dodoma Mei 30,
2017.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mhe.Faida Bakara akiuliza swali katika kikao
cha 37 cha Mkutanowa Saba wa Bunge la 11 leoMjini Dodoma Mei 30, 2017.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mhe.Amina Mollel akiuliza swali katika kikao
cha 37 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leoMjini Dodoma Mei 30, 2017.
Waziri wa Habari,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Dk.Harrison Mwakyembe akizungumza
jambo na Naibu wake Mhe.Anastazia Wambura katika kikao cha 37 cha Mkutano wa
Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 30, 2017
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge,Ajira,Kazi,Vijana na Watu
wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama akijadili jambo na Mbunge wa Iringa Mjini(CHADEMA)
Mhe.Peter Msigwa katika kikao cha 37 cha Mkutanowa Saba
wa Bunge la 11 leoMjini Dodoma Mei 30, 2017.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe.GeorgeMasaju akifafanua jambo katika kikao
cha 35 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 30, 2017.Kushoto
kwake ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Ajira,Kazi,Vijana na
Watu wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama na Kulia ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini
Dk.Medard Kalemani.
PICHA: SPIKA WA BUNGE ATEMBELEWA NA MCHUNGAJI LUSEKELO LEO MJINI DODOMA
Spika
wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (wa pili kushoto)akimsikiliza Mbunge wa Viti
Maalum, Mheshimiwa Anna Lupembe (aliesimama)akizungumza jambo pale ugeni kutoka
kanisa la Maombezi (GRC)ukiongozwa na Mchungaji, Anthony Lusekelo (wa pili
kulia)ulipomtembelea leo katika ukumbi wa Spika Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge,
Mheshimiwa Job Ndugai (katikati) akipiga picha ya pamoja na ugeni kutoka Kanisa
la Maombezi (GRC) ukiongozwa na Mchungaji Anthony Lusekelo (wa tatu kulia)
baada ya kikao kilichofanyika leo katika ukumbi wa Spika Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge,
Mheshimiwa Job Ndugai (katikati) akizungumza jambo wakati alipotembelewa na ugeni
kutoka Kanisa la Maombezi (GRC) ulioongozwa na Mchungaji Anthony
Lusekelo (wa pili kulia) katika kikao kilichofanyika leo katika ukumbi wa Spika
Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge,
Mheshimiwa Job Ndugai (wa pili kulia) akimsikiliza Mchungaji Anthony Lusekelo
(kulia) kutoka Kanisa la Maombezi (GRC) pale alipomtembelea leo katika ukumbi
wa Spika Mjini Dodoma.
SERIKALI KUIFANYIA MABADILIKO SHERIA YA NDOA NA MIRATHI
Thursday, 25 May 2017
WANNE WAFUKIWA NA KIFUSI NA KUFARIKI MKOANI GEITA
NHIF YAZINDUA MPANGO WA MADAKTARI BINGWA MKOANI GEITA
Kaimu Mkurugenzi wa tiba na
ushauri wa kiufundi NHIF Makao makuu ,Dr Aifena Mramba akielezea malengo ya
kuwepo kwa madkatari Bingwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita wakati
wa hafra fupi ya uzinduzi ambayo imefanyika kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa
huo.
Kaimu
Mkurugenzi wa tiba na ushauri wa kiufundi NHIF Makao makuu ,Dr Aifena Mramba
akimkabidhi Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita Celestine Gesimba Shuka mia moja
ambazo wametoa kama msaada kwa hosptali hiyo.
Meneja wa
NHIF Mkoani Geita Mathias Sweya Akitoa utambulisho mbele ya mgeni Rasmi wakati
wa Hafra fupi ya uzinduzi wa Mpango wa Madaktari Bingwa.
Mfuko wa Taifa wa Bima ya afya (NHIF) umezindua mpango wa madaktari Bingwa
Mkoani Geita lengo likiwa ni kushirikiana na serikali kupunguza
changamoto za upatikanaji wa huduma za kibingwa na kusogeza huduma karibu na
wananchi pamoja na wanachama wa mfuko huo.
PICHA: YALIYOJIRI KATIKA KIKAO CHA 34, MKUTANO WA SABA BUNGE LA 11 MJINI DODOMA LEO MAY 25, 2017
Mwenyekiti wa Bunge Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Najma Giga akiongoza kikao cha thelasini na nne cha
Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 25, 2017.
Waziri wa Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Jenista
Mhagama akiomba Bunge kutengua Kanuni zake na kuruhusu Bunge
kuhairisha shughuli zake saa kumi na mbili jioni ili kuruhusu wabunge ambao ni
waumini wa dini ya Kiislaamu kutimiza matakwa ya mfungo mtukufu wa Ramadhani
unaotarajiwa kuanza Jumamosi.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Vijana,Ajira na
Kazi Mhe. Anthony Mavunde akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao
cha thelasini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei
25, 2017.
Mhe. William Ole Nasha Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi akijibu
maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha thelasini na nne cha
Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 25, 2017.
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof Makame
Mbarawa na Naibu wake Mhe.Edwin Ngonyani wakijadiliana jambo katika kikao cha
thelasini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 25,
2017.
Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.William Lukuvi
akiwasilisha Makadirio ya Maapto na Matumizi ya Bajeti ya Wizara
yake kwa mwaka wa Fedha 2017/2018 katika kikao cha thelasini na nne cha Mkutano
wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 25, 2017.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Nchemba akizungumza jambo
na Mhe. Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dk. Philip Mpango katika kikao cha
thelasini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 25,
2017.
Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage
akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha thelasini na
nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 25, 2017.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt Hussein
Mwinyi akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha
thelasini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 25,
2017.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mbeya Mhe. Mary Mwanjelwa
akiuliza swali katika kikao cha thelasini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge
la 11 leo Mjini Dodoma Mei 25, 2017.
Mbunge Bukoba Vijijini Mhe. Jasson Rwekiza akiuliza swali katika kikao
cha thelasini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei
25, 2017.
Mbunge wa Mbulu
Vijijini Mhe. Flatei Massay akiuliza swali katika kikao cha thelasini na nne
cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 25, 2017.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Nchemba
akijadiliana jambo na Mbunge wa Arusha Mjini Mhe. Godbless Lema
Mbunge wa Arusha Mjini katika kikao cha thelasini na nne cha Mkutano wa saba wa
Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 25, 2017.
Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage
akijadiliana jambo na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Dkt Medard
Kalemani katika kikao cha thelasini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11
leo Mjini Dodoma Mei 25, 2017.
Mbunge wa Hanang Dkt Mary Nagu akiuliza swali katika kikao cha thelasini
na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 25, 2017.
Mbunge wa Ileje Mhe.Janeth
Zebedayo Mbene akiuliza swali katika kikao cha thelasini na nne cha Mkutano wa
saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 25, 2017.
Timu ya Mpira ya Mbao FC kutoka Mwanza wakifuatilia mijadala mbalimbali
Bungeni, Mbao Fc wapo Mjini Dodoma kwa ajili ya maandalizi ya Mchezo wa fainali
za FA kati yao na Simba Fc zitakazofanyika katika Uwanja wa Jamhuri Mjini
Dodoma Jumamosi ya May 27, 2017.
Mabingwa wa Ligi kuu
Tanzania Bara Dar Young African “Yanga” kwa msimu 2016/2017 wakifuatilia
mijadala mbalimbali Bungeni Mjini Dodoma.
Mabingwa wa Ligi kuu Tanzania Bara Dar Young African “Yanga” kwa msimu
2016/2017 wakifurahia na mawaziri na wabunge mara baada ya kulileta kombe la
Ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara Bungeni Mjini Dodoma.
Mbunge wa Mtwara Vijijini Mhe.
Hawa Ghasia akiuliza swali katika kikao cha thelasini na nne cha Mkutano wa
saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 25, 2017.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dk. Philip Mpango akijibu maswali
mbalimbali ya wabunge katika kikao cha thelasini na nne cha Mkutano
wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 25, 2017.
MAHENGE AVAA KIATU CHA ALPHONCE MAWAZO GEITA
Mwenyekiti aliyechaguliwa wa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA,Fabian Mahenge Akiomba kura kwa wajumbe wakati wa mkutano wa maamuzi ya uchaguzi wa ndani ya chama hicho. |
Mgombea wa uenyekiti Bw,Charles Makanje akiomba kuchaguliwa wakati wa uchaguzi wa mwenyekiti ngazi ya Mkoa ndani ya chama cha CHADEMA. |
Miongoni mwa wasimamizi wa uchaguzi huo,ambaye ni Afisa wa kanda wa chama Mayala Marthin Akionesha karatasi ya uchaguzi mbele ya wajumbe. |
Uchaguzi ukiendelea moja kati ya wajumbe akidumbukiza kikaratasi kwenye chombo cha uchaguzi. |
Uchaguzi ukiendelea moja kati ya wajumbe akidumbukiza kikaratasi kwenye chombo cha uchaguzi. |
Wajumbe wakifuatilia uchaguzi huo. |
Msimamizi wa uchaguzi ambaye ni Katibu wa kanda ya ziwa wa chama hicho,Bi Rehema James Mkoha akitangaza matokeo ya uchaguzi huo. |
Msimamizi wa uchaguzi ambaye ni Katibu wa kanda ya ziwa wa chama hicho,Bi Rehema James Mkoha,akimkabidhi hati ya ushindi Fabian Mahenge ambaye ndio mwenyekiti wa chama hicho ngazi ya Mkoa. |
Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Geita ,Fabian Mahenge akiwashukuru wajumbe kwa kumpigia kura na kumpa nafasi ya kuwaongoza ndani ya chama hicho. |
Chama cha
demokrasia na maendeleo (Chadema) Mkoani Geita kimefanya uchaguzi wa ngazi ya
mwenyekiti kwaajili ya kuziba nafasi ya aliyekuwa
mwenyekiti wa chama hicho,Mkoani humo Alphonce Mawazo aliyeuwawa mwezi wa kumi na moja mwaka 2015 huko kwenye Kijiji cha Ludete
Halmashauri ya mji mdogo wa katoro.
Uchaguzi huo
ulianza majira ya saa Sita na kumalizika saa kumi na moja jioni na msimamizi
akiwa ni Katibu wa kanda ya ziwa wa chama hicho,Bi Rehema James Mkoha ambaye
aliwatangaza wagombea wa kiti hicho kuwa ni Fabian Mahenge na Charles Makanje.
Hata hivyo
pamoja na kuwepo kwa figisu figisu kwa baadhi ya wajumbe kuonekana kutoa rushwa
Msimamizi wa uchaguzi aliwaonya wenye tabia za namna hiyo kuachana nazo mala
moja kwani uchaguzi huo unazingatia misingi ya haki kama ilivyo ndani ya katiba
ya chama hicho.
Bi,Mkoha
akiwa kama msimamizi wa uchaguzi huo alimtangaza Fabian Mahenge kuwa ni msindi
wa kiti hicho kwa kura 35 sawa ni asilimia 61.4 huku mgombea Mwingine
Bw,Charles Makanje akipata kura 22 sawa na asilimia 61.4.
Hivyo kutokana
na matokeo hayo Msimamizi wa uchaguzi huo alimtangaza Bw ,Fabian Mahenge
kuwa mrisi wa nafasi ya aliyekuwa
mwenyekiti wa chama hicho ngazi ya Mkoa Alphonce Mawazo aliyeuwawa tarehe 14
mwezi wa 11 mwaka 2015 na kuzikwa tarehe 30 mwezi wa 11 mwaka 2015.
Kwa upande
wake mwenyekiti ambaye amechaguliwa Bw,Fabiani Mahenge amewahidi wanachama kuwatumikia kwa kujitoa pamoja na kuwa na mshikamono huku
akikemea swala la matabaka ndani ya chama na kuwataka wanachama kuwa wamoja
katika kutetea masirahi ya chama hicho.
Uchaguzi huo
ulikuwa na idadi ya ya wapiga kura
waliojisajiri 59 ,idadi ya kura ambazo zimepigwa ni 57 halali 57 na ambao
hawakupiga kabisa ni 2.
Subscribe to:
Posts (Atom)