Tuesday 30 May 2017

SERIKALI KUIFANYIA MABADILIKO SHERIA YA NDOA NA MIRATHI



Serikali kupitia Wizara ya Afya,Maendeleo yaJamii,Jinsia,Wazee na Watoto imesema kuwa imewasilisha mapendekezo ya maboresho ya Sheria ya Ndoa na Sheria ya Mirathi Wizara ya Katiba na Sheria pamoja na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa hatua zaidi.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Afya Dkt.Hamis Kigwangalla wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mhe.Faida Bakar leo katika kikao cha 37 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 Mjini Dodoma.

Amesema kuwa katika kutokomeza ndoa za utotoni,mwaka 2016 Serikali iliifanyia marekebisho Sheria ya Elimu ya Mwaka 1978 ili kuzuia watoto wa shule wasiolewe ambapo kwa mujibu wa Sheria hiyo Na.4 /2016 kifungu cha  60 (A )hairuhusiwi mtu yeyote kuoa au kumpa ujauzito mwanafunzi wa shule ya msingi au Sekondari.

Aidha kwa kuwa Sheria hii inalenga zaidiu linzi kwa watoto walio mashuleni,bado ipo haja ya kuviondoa kabisa vifungu vinavyoruhusu ndoa za utotoni kwenye sheria ya ndoa kama ilivyofanyika kwa nchi nyingine kama vile Bangladesh,Yemen,Kenya na Malawi ilikuondoa mkanganyiko wowote unaoweza kujitokeza.

Ameeleza kuwa Sheria ya Ndoa yaMwaka 1971 katika kifungo cha 13 na 17, vinaruhusu mtoto wa kike kuolewa katika umri mdogo wa miaka 14 na 15 kwa ridhaa ya wazazi au Mahakama ambapo vifungu hivi humnyima mtoto haki zake za msingi.

“Pamoja na hayo pia Sheria za Mirathi za Kimila GN.379 na 436 za mwaka 1963 zimekuwa zikiwanyima haki za urithi na umiliki wa ardhi wanawake na watoto kwa ujumla”Alieleza Mhe.Kigwangalla.

Serikali imeamua kuleta miswada hii Bungeni ili kuboresha na kubadilisha sheria hizi ili ziendane na wakati na kuwapatia haki wanawake nawatoto.

No comments:

Post a Comment