Tuesday 30 May 2017

DC GEITA HERMAN KAPUFI - “MAHAKAMA NI MUHIMILI ULIO HURU”



Mkuu wa Wilaya ya Geita Mwl. Herman Kapufi amewataka wanasheria kuwasaidia wananchi kujua elimu ya sheria kutokana na wengi wao kushindwa kujua sheria hali ambayo inasababisha wengi kukosa haki zao za msingi pindi wanapofuatilia haki zao.
Hayo ameyasema wakati akifungua Taasisi isiyo ya kiserikali ya msaada wa kisheria ya “Himiza Social Justice” Wilayani hapa amesema elimu ya sheria na ushauri ni muhimu sana na kwamba kesi za migogoro ya ardhi  mirathi, kesi za jinai na madai ni nyingi kutokana na wengi kutokujua kesi hizo wanaweza kuzipeleka sehemu gani kwa ajili ya msaada.

Watu wengi ambao wamekuwa wakikwama kesi zao wamekuwa wakikimbilia kwenye ofisi ya mkuu wa Wilaya jambo ambalo ni ngumu kwa Mkuu wa Wilaya kuingilia kwani Mahakama ni chombo huru kisichoingiliwa na muhimili wowote  ule .

Mahakama ni muhimili ulio huru kumejengeka desturi ya baadhi ya wananchi Wilayani hapa kuja ofisini kwangu kuomba msaada wa kisheria jambo ambalo sio sahihi natoa Wito kwa wananchi kutambua kuwa huwezi kuingilia muhimili huu ni vyema wakawaoana wanasheria na mahakimu kwa msaada zaidi”Alisema Kapufi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi hiyo,Bernad Otieno,ameelezea kuwa kuanzishwa kwa taasisi hiyo ni kutokana na  kuwepo kwa  tatizo la msaada wa kisheria  hususani kwa watu wasiojiweza ikiwa ni pamoja na upungufu wa mawakili kwa maeneo ya vijijini.

“Vijana wachache Nikiwemo Mimi ,waliamua kuanzisha shirika hili walitamani na wanatamani kuongeza ubora wa upatikanaji wa haki katika jamii kupitia utoaji wa msaada wa kisheria ,ujenzi wa uwezo kwenye mambo ya kisheria na haki za biashara”Alisema Otieno.

Otieno aliongeza kuwa hadi Mwaka jana Tanzania Ilikuwa na sheria ya upande mmoja ya utoaji wa msaada wa kisheria iliyokuwa inajulikana kama The legal Aid(Criminal Proceesings)Act Cap.21(Kabla haijafutwa) ambayo kwa kiasi kikubwa ilikuwa ikisaidia utoaji wa msaada wa kisheria kwa kiasi kikubwa kwa watu wenye makosa ya mauaji ,sheria ambayo inatoa nafasi kwa watu wengine wanaoshitakiwa kwa makosa ya jinai kupata msaada wa kisheria.

“Huu ndiyo ulikuwa msukumo Mkubwa wa kuhakikisha jamii kubwa ya watu wa Geita na Tanzania Kwa ujumla hawawezi kumudu gharama za uwakilishi mahakamani na hata za kumuajiri wakili kwa shunghuli zao za kisheria” Aliongezea Otieno.


Hata hivyo baadhi ya wananchi Wilayani Humo,Eva Alex na Getruda Alias wamesema kufunguliwa kwa ofisi hiyo itatoa msaada mkubwa wa kisheria kwani ni muda mrefu wananchi wamekuwa wakikosa haki zao za msingi kutokana na kutokujua sheria hivyo ofisi hiyo itakuwa mwarobaini wa matatizo ya kisheria.

No comments:

Post a Comment