Friday 12 May 2017

MKUU WA MKOA WA GEITA AWEKA MAWE YA MSINGI KWENYE VITUO VYA AFYA VITATU,SHULE MOJA YA MSINGI NA MABWENI YA SEC KASAMWA

Mkuu wa Mkoa wa Geita,Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akiweka Jiwe la Msingi kwenye shule Mpya ya Msingi ya Tumaini Iliyopo kwenye Mtaa wa Nyantorontoro A Kata ya Nyankumbu Wilayani Geita.

Mkuu wa Mkoa wa Geita,Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akiweka Jiwe la Msingi kwenye shule Mpya ya Msingi ya Tumaini Iliyopo kwenye Mtaa wa Nyantorontoro A Kata ya Nyankumbu Wilayani Geita.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita Mhandisi Modest Aporinal akielezea  miradi iliyozinduliwa kuwa ni Fedha za mapato ya ndani ndio ambayo imeweza kufanya shughuli za ujenzi wa shule na vituo vya afya.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Geita,Leornad Kiganga Bugomola,,akizungumzia juu ya kutatua Kero za Afya,na elimu katika Halmashauri ambayo anaiongoza ambapo hadi sasa ni shule Moja Ambayo imekwisha zinduliwa kwaajili ya wanafunzi wa msingi kuanza masomo yao kutokana na umbali ambao walikuwa wakiupata wa kufuata elimu.

Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akiwasisitiza wananchi kuwa ni  watu wa kujitolea kwenye maendeleo na kuachana na itikadi za kisiasa ambazo zimekuwa zikirudisha jitihada za maendeleo  Nyuma.

Mkuu wa Mkoa wa Geita  akikagua chumba cha Darasa kwenye shule ya Msingi ya Tumaini.

Mkuu wa Mkoa Akiteta jambo na Mwenyekiti wa Halmashauri kutokana na kazi ambayo imefanyika kwenye halmashauri ya mji wa Geita.

Mkuu wa Mkoa akiwapongeza viongozi wa Halmashauri ya Mji wa Geita Mkurugenzi pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji kwa juhudi ambazo wamezifanya .

Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akiweka jiwe la Msingi kwenye kituo cha afya cha Mpomvu kilichopo kwenye Kata ya Mtakuja.

Mkuu wa Mkoa wa Geita akizungumza na wananchi baada ya kuweka jiwe la msingi kwenye kituo cha afya.



Kituo cha afya cha Nyanguku

Mkuu wa Mkoa pamoja na Diwani wa Kata ya Nyanguku Elias  Ngolle akionesha baadhi ya vyumba vya kituo cha afya.

Jiwe la Msingi la kituo cha afya cha Nyanguku.

Bwalo la chakula kwenye shule ya Sekondari ya Kasamwa ambayo pia Mkuu wa Mkoa aliweka jiwe la msingi wa ujenzi wa Bwalo pamoja na Mabweni.

Mkuu wa Mkoa wa Geita akiweka Jiwe la Msingi  Kwenye Mabweni  na Bwalo shule ya sekondari ya Kasamwa. 

Mkuu wa Mkoa wa Geita Akikagua baaadhi ya Mabweni kwenye shule ya Sekondari ya Kasamwa.

Baadhi ya Mabweni ambayo yanaendelea Kujengwa kwenye Sekondari ya Kasamwa .

Katibu wa Mbunge wa Geita Mjini ,Mariam Mkaka akiwasisitiza wanafunzi hususani ni wa kike kusoma kwa Bidii zaidi kutokana na kwamba serikali imetatua changamoto yao kwa kujenga Mabweni.





Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenereli  Mstaafu Ezekiel Kyunga amezindua na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi mitano ambapo mitatu ni vituo vya afya na viwili ni shule moja na Mabweni kwenye shule ya sekondari Kasamwa.


Akielezea Miradi hiyo yote Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji  Mhandisi Modest Aporinali  amesema bajeti ambayo waliyonayo kwa kila kituo cha afya wametenga kiasi cha sh ,Milioni Miamoja na kwamba mahitaji ni vituo vya afya kumi na kwasasa ni vituo viwili ambavyo vinafanya kazi.

“Ni kweli Halamshauri yetu inauwitaji Mkubwa sana wa Vituo vya afya ingawa kwa sasa tunavyo vituo viwili ambavyo ni Nyankumbu na Kasamwa ambavyo vinafanya kazi hata hivyo mmeona tumezindua na kuweka mawe ya msingi kwenye vituo vitatu ambapo ni Mpomvu,Nyanguku na Shiloleli tutaendelea na jitihada kwa kutumia mapato yetu ya ndani ili kupunguza changamoto ya vituo vya afya hata hivyo GGM wametupa msaada kama milioni mia moja kwaajili ya ujenzi wa kituo cha afya Mgusu”Alisema Modest.

Hata Hivyo Mkurugenzi Modest ametaja miradi ya shule ambazo zimewekewa mawe ya msingi kuwa ni shule ya Msingi Tumaini pamoja na Mabweni kwenye shule ya sekondari Kasamwa na kwamba wanaendelea na juhudi ya kupambana na changamoto za elimu kwenye Halmashauri ya Mji.

Mkuu wa Mkoa ,Meja jenerali mstaafu Ezekiel Kyunga ,amesisitiza kuwa serikali inafanya juhudi za kuwashirikisha wananchi katika swala la maendeleo na kwamba wanatakiwa kuwa na mwitikio katika swala la maendeleo kwa wao kama wananchi  kwa kujitolea bila ya kusubilia serikali huku akiwataka baadhi ya watu kutokuwa na desturi ya kulalamika bila ya kufanya shughuli kwa kushirikiana na Serikali.

Aidha kwa upande wao wananchi ambao wamezungumza na maduka online Habari wameipongeza serikali kwa hatua nzuri ya kuwapelekea vituo vya afya kwenye maeneo yao huku wakielezea changamoto ambazo zilikuwa zikiwakabili kabla ya kuwepo kwa vituo vya afya kuwa ni umbali mrefu wa kufuata huduma ya afya.

Jumla ya miradi yote ambayo imezinduliwa na kuwekewa mawe ya msingi imeghalimu kiasi cha Sh,Milioni Mia saba na thelasini na sita pesa ambazo zinatokana na mapato ya ndani.


No comments:

Post a Comment