Saturday 6 May 2017

OFISI YA MADINI MKOA WA GEITA YAMSIMAMISHA MWEKEZAJI WA KIGENI KUJENGA KIWANDA CHA KUCHENJULIA DHAHABU

Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Geita, Ali Said akizungumza ofisini kwake  juu ya hatua ya kumsimamisha mwekezaji kuendelea na ujenzi wa kiwanda cha kuchenjulia dhahabu . 
Wanakijiji  cha Ililika Kata ya Nyarugusu Wilayani Geita wakishirikiana kuziba Eneo la Bara bara ya kuelekea kwenye kiwanja ambapo ndiko ujenzi unaendelea.


Zikiwa ni siku Mbili zimepita tangu  wananchi wa Kjiji cha Ililika kata ya Nyarugusu  Wilayani Geita , kuandamana kupinga mwekezaji ambaye ni Raia wa China kuweka kiwanda cha  kuchenjulia dhahabu katikati  ya makazi yao na karibu na chanzo cha maji kijijini Hapo ,ofisi ya madini Mkoa wa Geita imemsitisha mwekezaji kuendelea na shughuli za ujenzi kwenye eneo hilo.


Akizungumza Ofisini kwake na mtandao wa maduka online , Afisa  Madini Mkazi Mkoa wa Geita, Ali Said ameitaja kampuni ya wachina iliyozuiliwa  kuwekeza Kiwanda cha kuchenjulia dhahabu kuwa ni JIN XIN, ambayo inaubia na Mtanzania.

amesema kuwa kutokana na malalamiko ya wananchi walikwenda kukagua na kujilizisha na kwamba wamemsimamisha mwekezaji kuendelea na mradi huo kutokana na malalamiko kutoka kwa wananchi wa kijiji hicho.

 “Tulipata taarifa ya kuandamana kwa wananchi kupinga mradi huo ambao mwekezaji anataka kuweka na sisi kama ofisi ya madini tumefika Kijijini hapo kwaajili ya kujilizisha na kweli tumegundua eneo sio rafiki hivyo tumezuia shughuli ya ujenzi kutokuendelea kwenye eneo hilo”Alisema Ali.

Katika hatua nyingine Afisa huyo amesema, mwekezaji yoyote anayewekeza kiwanda cha kuchenjulia dhahabu ni lazima apate ridhaa ya wananchi wa eneo husika.

“Kuna watu ambao wanashirikishwa kwenye swala la uwekezaji naamini ni serikali ya Kijiji na wananchi hivyo nadhani ni muhimu wananchi nao wakabariki kazi ambayo mwekezaji anaitaji kuweka nikiwa na maana ni swala la ushirikishwaji”Alisema Ali. 

Kwa upande wake Mjiolojia kutoka ofisi hiyo ya madini Godfrey Keraka, amebainisha madhara yakiwemo madhara ya kiafya ambayo yanaweza kuwapata wananchi wa maeneo hayo pamoja na makelele ya kiwanda vikiwemo vyanzo vya maji kuharibiwa.

Maduka Online imefika kwenye ofisi za afisa Mazingira wa Wilaya Hiyo Bi,Helen Eustace ambapo amesema kuwa wao kama ofisi hawana taarifa yoyote ya Mwekezaji Huyo na Kwamba wataakikisha wanafuatilia ili kuchukua hatua za kiafya na kimazingira.




No comments:

Post a Comment