Wednesday 17 May 2017

WAMILIKI WA MAGARI MKOANI GEITA KUTOPANDISHA NAULI KIHOLELA



Baadhi ya wamiliki wa magari ya usafirishaji  wa abiria katika vituo  mbalimbali  mkoani geita wametakiwa kuacha  mara moja tabia ya kujichkulia  sheria mkononi na kupandisha viwango vya nauli kinyume na vile vilivyopangwa na mamlaka ya usafiri wa nchi kavu na majini (SUMATRA).
Akizungumza na  storm habari Kaimu Afisa leseni mkoa wa Geita Bw. william haule  amesema kuwa vitendo hivyo vimekuwa vikifanywa na baadhi ya madereva pamoja na mawakala wa vyombo  hivyo vya usafiri kinyume na utaratibu wa mamlaka ya usafiri wa nchi kavu na majini SUMATRA.

katika hatua nyingine Bw haule  amesema kwa mmiliki yeyote wa chombo cha usafiri atakae bainika  kukutwa  na tuhuma hiyo ya kupandisha viwango vya nauli pasipo kufuata utaratibu kutoka sumatra  hatua kali za  kisheria zitachukuliwa dhidi yake ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani.

kwa upande  wake mwenyekiti wa chama cha madereva  mkoani hapa Bw. Faustini John  amekili kuwepo  kwa vitendo hivyo kwa baadhi ya madereva katika vituo mbalimbali mkoani hapa.
Bw. faustini amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa vyombo husika ili kuweza kuwabaini watu wanaojihusisha na tabia hiyo ya kupandisha viwango vya nauli.


Bw. Ahamad  Ahamed  na Jumanne Ally wao ni miongoni mwa mawakala  wa magari ya abiria katika kituo cha magari  cha geita mjini ambapo wameeleza  kuwa  abiria wanatakiwa  kuwa makini pindi wawapo  katika  vituo  vya magari kwani vitendo hivyo  vimekuwepo  na hufanywa na watu wasiyo kuwa wahusika wa magari hayo.

No comments:

Post a Comment