Wednesday 3 May 2017

GEITA YAADHIMISHA SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI




Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya  Geita,Ali Kidwaka akisisitiza waandishi kuwa na umoja na mshikamano katika kutetea na kulinda haki zao za msingi kwenye shughuli ambazo wanazifanya  Hayo ameyasema leo kwenye siku kuu ya uhuru wa Vyombo vya habari ambayo yamefanyika kwenye ukumbi wa Seft Park Mjini Geita.


Mkuu wa Wilaya ya Geita Mwl,Herman Kapufi akizungumza na waandishi wa Habari juu ya umuhimu wa Siku hiyo.


Waandishi wa habari na viongozi mbali mbali wakiwa kwenye Picha ya pamoja wakati wa maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya Habari.
Waandishi wa habari Wilayani na  Mkoani Geita  wametakiwa kuandika habari zenye ubora na zenye kuleta chachu ya maendeleo katika jamii.

Wito huo umetolewa na  Mkurugenzi Mtendeji wa halmashauri ya Wilaya ya hiyo Bw Ali Kidwaka wakati wa sherehe za  Maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Vyombo vya habari yaliyofanyika  ki Mkoa mjini Geita .

Amesema ili kuleta maendeleo katika Taifa na jamii kwa ujumla waandishi wa habari wanapaswa kuandika habari zenye ubora na zisizokuwa na upendeleo ambazo zitasaidia kwa kiasi kikubwa watu kujitambua katika kuleta maendeleo ya Taifa na Jamii kwa ujumla.

Pia amewataka kuendeleza ushirikiano na taasisi mbalimbali  ili kuweza kuibua changamoto  ambazo zitaleta maendeleo.

Kwa upande wake Mgeni rasmi katika sherehe hizo ambaye pia ni mkuu wa Wilaya hiyo,Mwl Herman Kapufi amesema kuwa ni vyema kwa waandishi kutumia muda mwingi wa kujifunza maeneo ambayo kwao bado yanautata pia kuwa wazalendo na kushikamana kwa pamoja

Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Geita Daniel Limbe amempongeza mkuu wa Wilaya ya Geita Pamoja na wadau wengine kuwa bega kwa bega katika kuwasaidia waandishi ambao wapo wilayani Geita.

 “kauli mbiu ya maadhmisho hayo ni  klabu za waandishi wa habari zina wajibu wa kuendeleza amani katika jamii” ambapo Kitaifa yameadhimishiwa Jijini Mwanza.


No comments:

Post a Comment