
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Joseph Kabila akipokelewa
na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli
wakati alipowasili katika jengo la Mamlaka ya Bandari ya Tanzania kwa ajili ya
kuweka jiwe la msingi mapema hii leo jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Joseph Kabila kushoto
pamoja na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Magufuli wakitoa heshima kwa wimbo wa Taifa wakati wa sherehe za kuwekaji jiwe
la msingi katika Jengo la Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) mapema hii leo
jijini Dar es Salaam ambapo Rais wa Kabila alikuwa mgeni rasmi.

Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania Bw. Deusdedit Kakoko akitoa
neno la utangulizi kwa Marais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Joseph
Kabila na wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli (hawapo
pichani) wakati wa sherehe za kuwekaji jiwe la msingi katika Jengo la Mamlaka
ya Bandari Tanzania (TPA) mapema hii leo jijini Dar es Salaam ambapo Rais wa
Kabila alikuwa mgeni rasmi.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akielezea
historia fupi ya mradi “One Stop Centre” ulio chini ya Mamlaka ya Bandari
Tanzania (TPA) kabla ya sherehe za uwekaji jiwe la msingi uliofanywa na Rais wa
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Joseph Kabila mapema hii leo jijini Dar
es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli akisisitiza
jambo kwa wafanyakazi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) pamoja na wageni
mbalimbali waliohudhuria sherehe za kuwekaji jiwe la msingi katika Jengo la
Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) mapema hii leo jijini Dar es Salaam ambapo
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Joseph Kabila alikuwa mgeni
rasmi.

Baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na
Wakandarasi wa Jengo la Mamlaka hiyo wakimskiliza kwa makini Mgeni Rasmi Rais
wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Joseph Kabila wakati alipokuwa
akielezea nia ya nchi yake kuitumia bandari ya Dar es Salaam mapema hii leo
wakati wa uzinduzi wa jengo la kitega uchumi la mamlaka hiyo “One Stop Centre”
mapema hii leo jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Joseph Kabila akielezea
dhamira ya nchi yake kuitumia bandari ya Dar es Salaam kwa wafanyakazi wa
mamlaka hiyo (hawapo pichani) wakati wa sherehe za kuwekaji jiwe la msingi
katika Jengo la Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) mapema hii leo jijini Dar es
Salaam ambapo Rais wa Kabila alikuwa mgeni rasmi.

Rais wa Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Joseph Kabila akifunua kitambaa kuashiria uzinduzi
rasmi wa jiwe la msingi katika jengo la kitega uchumi la Mamlaka ya Bandari
Tanzania “One Stop Centre” mapema hii leo jijini Dar es Salaam ambapo Rais wa
Kabila alikuwa mgeni rasmi.
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Joseph Kabila na mwenyeji
wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli wakiwa katika
picha ya pamoja na Mabalozi pamoja na Mawaziri toka Kongo (DRC) na Tanzania.
No comments:
Post a Comment