Monday 17 October 2016

GGM YAFADHILI MILIONI 20 KWA AJILI YA MAKTABA KATIKA SHULE YA NYANKUMBU




Mkuu wa Wilaya ya Geita,Herman Kapufi akizindua maktaba ya kisasa iliyopo shule ya wasichana ya nyakumbu iliyopo kata ya Nyakumbu.


Msemaji wa shirika lisilo la Kiserikali la Read International Stella Mtega,akishukuru kwa GGM kwa kufanikisha kutoa fedha ambazo zimesaidia kununua vitabu kwaajili ya maktaba.


Afisa mahusiano wa GGM Manase Ndoloma akiwaeleza wanafunzi  wa shule ya  sekondari ya wasichana  nyakumbu umuhimu wa kupenda kusoma vitabu ni kwenye uzinduzi wa maktaba katika shule hiyo ulio fanyika leo tarehe 17 Oktoba.

Jumla ya kiasi cha sh milioni ishirini (20) kimetolewa na mgodi wa dhahabu wa Geita (GGM) kwenye shule ya Sekondari ya wasichana ya Nyankumbu iliyopo wilayani na mkoani Geita lengo ikiwa ni kuweka vitabu vya kutosha katika maktaba ya  shule hiyo.

Akizungumzia changamoto ambazo walikuwa wakikutana nazo wanafunzi wa shule hiyo,Hajira Salum na Verediana Traphone wamesema kuwa changamoto ya uhaba wa vitabu shuleni hapo ilikuwa ni moja wapo  ya kikwazo kilichokuwa kikisababisha wanafunzi kutokufanya vizuri shuleni hapo .

Aidha kwa upande wake  Afisa mahusiano ya jamii wa mgodi wa GGM Manase Ndoroma,amewasisitiza wanafunzi hao kujenga desturi ya kusoma kwa bidii vitabu ili kuendana na Dunia ya sayansi na teknolojia.

“Tunatambua kuna faida nyingi sana katika kusoma vitabu, hivyo ni muhimu nyie wanafun zi kutumia maktaba hii kwa kusoma vitabu vingi zaidi kwani kuna mambo mengi mazuri katika kujisomea  na tuombe mashirika mengine ni vyema yakajitokeza kuchangia maendeleo ya elimu nchini”Alisema Manase.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo,Georgia Mgashe,amefafanua  kuwa vitabu hivyo vitakuwa   msaada mkubwa kwa shule hiyo kwani hakutakuwa na kisingizio cha kukosekana kwa vitabu shuleni hapo .

“Imani yangu ni kwamba kwa sasa wanafunzi watasoma kwa bidii na kujituma zaidi kwani hakuna kisingizio cha kukosekana kwa vitabu tumeona GGM wameweka vitabu vingi katika maktaba yetu”Alisema Mgashe.

Msemaji wa Read internation  Stella  Mtega ,ametoa shukrani kwa mgodi wa dhahabu wa GGM kwa kuwezesha ufadhili  vitabu vingi katika maktaba hiyo.

Akizindua Maktaba hiyo Mgeni rasmi ambae ni mkuu wa wilaya ya Geita mh Herma Kapufi amewasisitiza wanafunzi kutunza vifaa  na vitabu vilivyonunuliwa ili viweze kuja kutumiwa na wanafunzi wengine.

No comments:

Post a Comment