Na.Joel Maduka
Waziri wa
Kilimo Dr Charles Tizeba amewataka wamiliki wa viwanda vya kuchambua pamba
kupeleka mbegu za Pamba kwenye kiwanda cha kuzitolea manyoya cha Q-Ton na
kwamba watakaokiuka hawatanunua Pamba msimu ujao.
Akizungumza
na wadau wa pamba mkoani Geita, Dr Tizeba amesema atakayeshindwa kupeleka mbegu
kwenye kiwanda cha kuzichakata, hatafanya biashara hiyo tena.
“Najua kuna maginner wanne hapa sasa atakayegoma kupeleka pamba mbegu Q-ton hanunui
pamba mwaka kesho, wanapaswa kupeleka mbegu zitolewe manyoya ziende kwa wananchi ili
wapate mbegu bora, katika hili sitabembelezana na mtu” alisisitiza Tizeba.
Alisemesema
serikali ya kijiji ni vyema ikasimamiwa kikamilifu na halmashauri husika wakati
wa ugawaji wa mbegu kutokana na kuendelea kwa malumbano yasiyo mazuri kwenye
shughuli za kilimo cha pamba.
Mkuu wa Mkoa
wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga amezitaka Halmashauri kuwajibika
kuhakikisha zinabeba dhamana ya kilimo cha mkataba kwa Mkulima.
Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Bukombe Nicas Mayala amesema wako tayari kutekeleza agizo
hilo la waziri wa kilimo.
No comments:
Post a Comment