Wednesday 25 October 2017

WAKAZI WA CHIKOBE GEITA WALALAMIKIA KUCHELEWA KWA MRADI WA MAJI




Mabomba ambayo yanatoka kwenye mradi wa Nchakolongo yakiwa yametandazwa wakati Mkuu wa Wilaya ya Geita alipokwenda kutembelea na kukagua maendeleo ya mradi  pamoja na wataalam.


Chanzo cha maji ambacho ndio kinatumiwa  na wanakijiji wa kijiji cha Chikobe. 


Mkuu wa Wilaya ya Geita ,Mwl Herma Kapufi akizungumza na wananchi wa kijiji cha Chikobe juu ya hatua ambazo zinaendelea kutekelezwa na serikali ili kumaliza mradi huo na tatizo la maji kwenye kijiji hicho. 

Wakazi wa Kijiji cha Chikobe Kata ya Nyachiluluma wilayani Geita wanakabiliwa na tatizo la maji hali inayohatarisha afya zao kwa kutumia maji yasiyo safi na salama. 

Wakizungumza  wakati wa Mkutano wa hadhara baadhi ya wananchi hao Bi Pili Simon Goi na Maganga Paul Walisema kuwa wamekuwa wakitumia muda mrefu kutafuta maji na kwamba kumekuwa na mabomba yanayowekwa bila kutoa maji huku kukiwa na mradi wa maji ulioanza mwaka (2010 )lakini haujakamilika hadi sasa.

“Sisi wakina mama ndio wahanga wakubwa  ukosekanaji wa maji kwani tumekuwa tukiamka usiku wa manane kwenda kutafuta maji na muda mwingine tunakuwa na hofu kubwa kutokana na kuogopa kufanyiwa vitendo vya ukatili likiwemo swala la kubakwa kwakweli tunatesekan Sana”Alisema Bi,Pili Goi.

“Kuna mradi ambao umeanzishwa tangu mwaka 2010 lakini jambo la kusikitisha hadi sasa mradi huo ujakamilika na tunapata shida ya maji tunaomba serikali itusaidie juu ya swala hili”Alisema Maganga Paul.

Akizungumza kwenye Mkutano huo wa hadhara Mkuu wa Wilaya ya Geita Mwl Herman Kapufi aliwataka wakazi wa kijiji hicho kuwa wavumilivu kwa kuwa tatizo hilo litapatiwa ufumbuzi muda mfupi ujao.

Kaimu mhandisi wa maji wa Wilaya ya Geita Bw Yusuf  Chalamanda alisema mradi wa maji wa Nchankolongo umechukua muda mrefu kutokana na tatizo la fedha na baadhi ya wakandarasi kutokuwa waaminifu na kwamba  wanatarajia kuanza kufanya  majaribio kwa kusambaza maji kwenye vijiji vya Chikobe, Nchankolongo, Chiguga na Kabayozo na pia mradi huo  utakamilika na kuanza kusambaza maji rasmi Desemba 12 mwaka huu.


No comments:

Post a Comment