Translate message
Turn off for: Swahili
PICHA NA JOEL MADUKA
Ukosefu wa walimu
wa sayansi imeelezwa
kuwa ni kikwazo ambacho
kimesababisha wanafunzi wengi
kutokuwa na mwamko wa masomo hayo
na kujikuta wengi wao wakikimbilia kwenye
masomo ya sanaa.
Hayo yamebainishwa na
mwalimu wa shule ya sekondari ya Senga
Mwl,Magoma Komesi Magero kwenye mahafali
ya nne,amesema pamoja
na shule hiyo kuendelea kufanya vizuri kwenye mitihani ya Kitaifa na
mtihani wa utimilifu bado inakabiliwa na
changamoto ya walimu
wa masomo ya Baioloji na kemia.
Akisoma Risala kwa mgeni rasmi ambayo iliandaliwa na
wanafunzi wa Kidato cha nne, Venasia Frances Amesema shule hiyo inawalimu wa masomo ya sayansi
watano tu ukilinganisha na idadi ya wanafunzi ambao wapo shuleni hapo huku
akigusia na swala la vyumba vya madarasa.
Mgeni rasmi kwenye
mahafali ,Mkuu wa Wilaya ya Geita Mwl Herman Kapufi,ameitaka halmashauri
kuongezea walimu wa masomo ya sayansi na pia amewapongeza walimu hao watano wa
masomo ya sayansia pamoja na uchache wao wamejitahidi kufanya vizuri kwenye
masomo hayo.
Jumla ya
wanafunzi ambao wamesajiliwa
kufanya mtihani kwenye shule ya sekondari ya Senga
ni 97.
No comments:
Post a Comment