Monday 23 October 2017

PICHA: RAIS JOHN MAGUFULI AWATUNUKU VYETI WAJUMBE KAMATI ZA MAKINIKIA



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Mke wa Spika Bibi. Fatma Ndugai kwa niaba ya Spika Job Ndugai ikiwa ni cheti cha utambuzi wa mchango wake katika kusimamia rasilimali za nchi hasa madini katika hafla ya kuwatunuku vyeti wajumbe wa Kamati zilizohusika katika sakata la Makinikia leo Ikulu Jijini Dar es Salaam. Katika ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi na Katibu wa Bunge Stephen Kagaigai.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi cheti cha kutambua mchango wake katika kusimamia rasilimali za nchi mjumbe wa kamati zilizoshughulikia masuala ya Makinikia ambaye pia ameteuliwa kuwa Gavana wa Benki Kuu (BOT) Profesa Florens Luoga  wakati wa  hafla ya kuwatunuku vyeti wajumbe wa Kamati zilizohusika katika sakata la Makinikia leo Ikulu Jijini Dar es Salaam. Katika ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi. 

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi cheti cha kutambua mchango wake katika kusimamia rasilimali za nchi mjumbe wa kamati zilizoshughulikia masuala ya Makinikia Bibi. Monica Philip  wakati wa  hafla ya kuwatunuku vyeti wajumbe wa Kamati zilizohusika katika sakata la Makinikia leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.



Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) aliyeteuliwa  leo kushika wadifa huo Profesa Florens Luoga akisalimiana na Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Juma Zuberi katika hafla ya kuwatunuku vyeti wajumbe wa Kamati zilizohusika katika sakata la Makinikia leo Ikulu Jijini Dar es Salaam. Nyuma ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi William Lukuvi akisalimiana na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Mussa Salum.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Haruna Lipumba  walipokutana katika hafla ya kuwatunuku vyeti wajumbe wa Kamati zilizohusika katika sakata la Makinikia leo Ikulu Jijini Dar es Salaam. 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Mawaziri na waliokuwa wajumbe wa Kamati zilizoshugulikia suala la Makinikia wakati wa  hafla ya kuwatunuku vyeti wajumbe hao leo Ikulu Jijini Dar es Salaam. 


No comments:

Post a Comment