Thursday 10 August 2017

WATANZANIA WATAKIWA KUJENGA DESTURI YA KUTHAMINI BIDHAA NA HUDUMA ZA NDANI YA NCHI



Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Kitaifa,Amour Hamad Amour,amewataka Watanzania kujenga desturi ya kupenda kununua Bidhaa  ambazo  zinatengenezwa  na kuzalishwa hapa Nchini  kwaajili ya kuendelea kuwanyanyua wajasiriamali  wadogo pamoja na kuinua kipato cha Nchi.hapa ni wakati alipokuwa akionesha kitenge ambacho kimetengenezwa nchini.




Mradi wa usambazaji wa maji ambao upo kijiji cha Kiliman



Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Kitaifa,Amour Hamad Amour,akiweka jiwe la Msingi kwenye mradi wa maji



Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Kitaifa Amour Hamad Amour amewataka Watanzania kujenga desturi ya kupenda kununua Bidhaa  ambazo  zinatengenezwa  na kuzalishwa hapa Nchini  kwaajili ya kuendelea kuwanyanyua wajasiriamali  wadogo pamoja na kuinua kipato cha Nchi
Rai hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizindua klabu ya mapambano dhidi ya ukimwi kwenye shule ya Sekondari ya Zhakia Meghji iliyopo Wilayani Chato Mkoani Geita,amesema kuwa Mikakati ya serikali ya kuhakikisha kwamba wanakuza uchumi wa Taifa haitawezekana endapo kama watanzania awatajari bidhaa ambazo zinatoka nchini Hapa.

 Aidha Amour ameendelea kusema  kuwa katika kuhakikisha nchi inakuwa ni ya maendeleo ni lazima kuwepo kwa mikakati thabiti ya kupambana na mambo ambayo yamekuwa yakirudisha Nyuma maendeleo likiwemo swala la uvivu,maradhi na vitendo ambavyo vinakiuka misingi ya Nchi.


Sanjali na hayo Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa ,ameweza kutembelea na kuweka jiwe la Msingi kwenye mradi wa usambazaji maji ambao upo kwenye Kijiji cha mlimani.

Akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi huo ,kaimu mhandisi  wa maji kwenye Halmashauri hiyo Mali Msango ,amesema kuwa mradi huo umeanzishwa kwa lengo la kuwapatia maji safi na salama na zaidi ya wananchi elfu ishirini na tano wananufaika na mradi huo.

Wakazi wa Chato,Maria Malare na Richard Bagolele,wamesema kuwa kuwepo kwa mradi huo na kuongezwa kwa Matanki imeleta msaada Mkubwa sana kwani walikuwa wakipata shida hapo awali Tofauti na sasa.


Miradi ambayo imepitiwa ni 12 na ambayo imezinduliwa ni  saba,minne imetembelewa na mmoja utawekewa jiwe la msingi ambapo miradi yote ina thamani ya   shilingi ,2,042,896,037.50 kati ya fedha hizo wahisani wamechangia shilingi,1,255.611.875,serikali kuu 691.808.162.50 halmashauri 91.020.00 na wananchi shilingi 4.456,000.

No comments:

Post a Comment