Thursday 3 August 2017

MKOA WA GEITA UNAKABILIWA NA UPUNGUFU WA WALIMU KWA SHULE ZA MISINGI


Mkoa wa Geita unakabiliwa na upungufu wa walimu elfu 13 na 577 huku waliopo wakiwa elfu 8 na 568 wa shule za msingi mkoani humo hali inayosababisha uwiano kati ya walimu na wanafunzi kushuka kuanzia Mwaka 2013 hadi sasa
Imeelezwa kuwa wanafunzi 31 wa shule za msingi na 196 wa Sekondari wamekatisha masomo baada ya kupata ujauzito kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2013 mpaka sasa.

Akisoma taarifa ya maendeleo ya Elimu Mkoani Geita katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya Elimu ngazi ya Mkoa, Afisa Elimu Mkoani humo Rehema Mbwilo amesema wilaya yenye upungufu mkubwa wa walimu ni Bukombe yenye upungufu wa asilimia 49

Kaimu Katibu tawala wa Mkoa huo Bw Emily Kasagala amewasisitiza wanafunzi kupenda Elimu na kuachana na utoro unaoweza kusababisha kuzorta kwa viwango vyao kitaaluma


Baadhi ya wanafunzi mkoani Geita Loveness Majaliwa na Rehema Joseph  wameiomba serikali kutatua changamoto za kielimu zilizopo ili wawe na mazingira mazuri ya kujifunzia huku kaimu mkuu wa mkoa wa Geita Bw Herman Kapufi akiahidi kushughulikia changamoto hizo.

No comments:

Post a Comment