Thursday 15 December 2016

HUMPHREY POLEPOLE AELEZA MIKAKATI YAKE BAADA YA KUKABIDHIWA OFISI NA NAPE NNAUYE



Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Humphrey Polepole amesema atahakikisha chama hicho kinakuwa ni cha wanyonge na kuendelea kuwa kimbilio la wasio na sauti.
Polepole ametoa kauli hiyo leo wakati akikabidhiwa rasmi ofisi na  Katibu anayemaliza muda wake Nape Nnauye katika ofisi ndogo za Makao Makuu ya chama hicho Lumumba jijini Dar es Salaam.

Polepole alisema kwa misingi ya chama hicho imejengwa kuwasaidia na kuwa tete wanyongo hivyo katika muda wake wa uongozi atahakikisha chama kinasimama katima misingi hiyo ya kuanzishwa kwake.

“Msingi wa chama chetu ni utetezi wa wanyonge, tutahakikisha kinaendelea kuwa kimbilio la wasio na sauti,” alisema Polepole.

Aidha, katibu huyo alisema kuwa katika kutekeleza majukumu yake aliyokabidhiwa leo na mtangulizi wake, atahakikisha anajikita zaidi katika kazi za itikadi zaidi kuliko uenezi kwa kuwa itikadi ndiyo inayokibeba chama.

Polepole alitumia muda huo kumshukuru Nape Nnauye anayemaliza muda wake na kusema kuwa ni kiongozi imara na kuwa katika muda wake aliweza kuitumikia vyema nafasi yake. Lakini pia alisema japo anamaliza muda wake, lakini atakuwa akimuhitaji mara kwa mara kwa ajili ya ushauri na mambo mengine.


Wakati huo huo, Polepole amemshukuru Mwenyekiti wa CCM Dkt John Pombe Magufuli na Halmashauri Kuu ku kumwamini na kumpa majukumu hayo makuwa.

No comments:

Post a Comment