Wednesday 28 March 2018

WANANCHI WATAKIWA KUNUNUA HISA NA HATI FUNGANI ILI KUNUFAIKA KIUCHUMI

Baadhi ya wadau wakiwa kwenye mafunzo ya ununuzi wa hisa ambayo yamefanyika kwenye ukumbi wa maarifa ya Nyumbani Mjini Geita.

Meneja Mahusiano ya Umma wa CMSA Bw Charles Shirima akifundisha namna ya uwekezaji wa hisa. 



Serikali kupitia mamlaka ya masoko ya dhamana na mitaji nchini ya Capital Markert and Securities Authority, CMSA imesema ununuzi na uuzaji wa hisa na Hati fungani za makampuni na serikali ni mbinu nzuri za kujiwekea akiba na kumfanya mtu kutajirika.
Hayo yamesemwa na Meneja Mahusiano ya Umma wa CMSA Bw Charles Shirima alipozungumza kwenye mafunzo ya siku moja yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa  maarifa ya Nyumbani Mjini Geita yaliyoshirikisha wananchi, wajasiriamali na wanafunzi wa shule za sekondari na vyuo Mjini Geita.


Amesema wajasiriamali na wananchi kwa ujumla wakiwa na tabia ya kuweka akiba kwa kununua Hisa za makampuni mbalimbali ya kibiashara wanaweza kupata utajiri kwa njia ya kupata gawio kila mwaka baada ya kampuni husika kupata faida na kugawa faida kwa Wanahisa wake.

Ametaja baadhi ya makampuni amabayo yanafanya vizuri zaidi hadi sasa kwenye soko la Hisa na kutoa gawio la faidi kwa wanahisa wake kuwa ni pamoja na Tanzania Breweries Limited(TBL),TOL Gases Limited,NMB Bank,CRDB Bank,Tanzania Tea Packers Limited,Tanzania Cigarette Company naTanga Cement Company Limited.


Amesema, mbali na gawio la faida ya kila mwisho wa mwaka baada ya kampuni kupata faida,mmiliki wa Hisa anaweza kuuza hisa zake muda wowote na kupata faida baada ya kugundua kuwa kipindi hicho Hisa za kampuni hiyo zimepanda bei kwenye soko la hisa.


Akifunga mafunzo hayo Kiongozi kutoka kwenye Taasisi ya maendeleo ya vijana na ushirikiano Tanzania  Aloyce Masana,aliishukuru sana CMSA kwa kutoa mafunzo hayo kwani wafanya biashara wengi walikuwa hawajui kama Hisa na Hati fungani ni uatijiri uliofichika.

No comments:

Post a Comment