Thursday 15 March 2018

GARI YACHOMWA MOTO NA WANANCHI MKOANI GEITA BAADA YA KUMGONGA MTU





Gari aina ya  lori lenye namba za usajili T415 DJG  limechomwa moto baada ya kumgonga mwendesha pikipiki  na kusababisha  kifo  cha Matha Paulo aliyekuwa ni Muuguzi wa kituo cha afya cha Kaseme Wilayani Geita alikuwa amebebwa kwenye pikipiki hiyo.

Tukio hilo limetokea majira ya saa moja jioni  katika kijiji cha Kasesa kwenye barabara ya katoro-Lunzewe ambapo mwendesha boda boda na abiria wake walikuwa wakitokea mji mdogo wa Katoro,huku watoto wawili kikiwepo kichanga cha miezi miwili waliokuwa wamepakatwa na marehemu mama yao wakinusulika kifo.

Akisimulia shuhuda wa tukio hilo Bw,Mayala Bushibe, amesema yeye alikuwa ameongozana na bodaboda iliyopata ajali,huku nyuma na mbele yao yalikuwapo magali mawili likiwemo lori yakipishana na boda boda alipojaribu kulipita ndiyo likawagonga gari hilo.

Josia Thobias ambaye ni mkazi wa Kaseme  na Tarafa Maganga  wamesema tukio la namna hiyo sio la mala ya kwanza kutokea kwani  ajali za hivyo zimeendelea kujitokeza na kwamba ni mala ya pili kutokea.


Kamanda wa polisi mkoa wa Geita Mponjoli mwambulambo amedhibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa pikipiki ambaye alikimbia baada ya kutokea kwa ajali,huku akiwataka wananchi kuachana na vitendo vya kujichukulia sheria mkononi.

No comments:

Post a Comment