Monday 5 March 2018

KANYASU AWAKINGIA KIFUA WAENDESHA BASKELI KUONDOLEWA MJINI

Mbunge wa jimbo la Geita mjini,Constatine Kanyasu akizungumza na wananchi wa mtaa wa msalala road kata ya kalangalala wakati wa mkutano wa kusikiliza kero za wananchi.

Mbunge wa jimbo la Geita mjini,Constatine Kanyasu akifurahia pamoja na wakina mama ambao walikuwa wakiimba kwenye mkutano huo.

Katibu wa itikadi na uenezi wa chama cha mapinduzi(CCM)Kata ya kalangalala,Richard Nzagamba akizungumza na wananchi wakati wa mkutano wa mbunge wa jimbo la Geita mjini.
Mwenyekiti wa mtaa wa Msalala road,Sostenes Calist Idory akielezea kero za ubovu wa mabarabara kwenye mtaa mbele ya Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini.



Katibu wa UVCCM Wilaya ya Geita,Ally Rajabu akielezea namna ambavyo waendesha Baiskeli walivyoondolewa katikati ya mji kufanya shughuli zao za kila siku.

Diwani wa kata ya Kalangalala ,Sospeter Mahushi akifurahia na wananchi wakati wa mkutano wa mbunge wa jimbo la Geita mjini.

Diwani wa kata ya Kalangalala ,Sospeter Mahushi  akizungumza na wananchi wakati wa mkutano wa mbunge wa jimbo la Geita mjini ambao ulikuwa na lengo la kusikiliza kero za wananchi.



Mbunge wa jimbo la Geita mjini Constantine Kanyasu, amepinga tamko la mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya mji wa Geita Mhandisi Modest  Apolinary  alilolitoa  hivi karibuni akiwataka wasafirishaji wa abiria kwa kutumia Baiskeli maarufu kwa jina la Daladala kusitisha shughuli hizo mjini Geita kwa madai kuwa wamekuwa chanzo cha ajali mjini humo.
Bw. Kanyasu akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wakati akisikiliza na kujibu kero za wananchi wa mtaa wa Barabara ya Msalala Kata ya Kalangalala alisema kuwa muda wa kuwazuia waendesha baiskeli kutoa huduma hiyo haujafika bali waendelee kufanya kazi bila kubughudhiwa .

Alisema kuwa aliyetoa tamko la kuwazuia waendesha Baiskeli hao kwa madai kuwa wanasababisha ajali mjini  hakufanya utafiti na kwamba hakuna kikao cha Baraza la madiwani kilichoketi na kukubaliana kuwa waendesha baiskeli hao maarufu Daladala wasitishe kutoa huduma hiyo mjini hivyo wataendelea kutoa huduma ya kubeba abiria kama kawaida.

Bw Kanyasu alisema kuwa mji wa Geita unakuwa lakini  yeye  binafisi amefanikiwa kufika China licha ya kupiga hatua kubwa kimaendeleo pamoja na teknolojia wananchi wa Taifa hilo bado kwenye barabara zao wanaendesha baiskeli hivyo bajaji na Pikpiki maarufu kama bodaboda pamoja na daladala waendele  kufanya kazi kwa kufuata sheria za barabarani kwa kuwa wote wana haki ya kutafuta riziki kwa kutumia kazi zao.

 ''Waendesha daladala za baikeli, Bajaji na waendesha Pikipiki wote wana haki ya kufanya kazi, aliyetoa tamko la kuzuia baiskeli hakufanya utafiti kwanza na hakuna kikao chochote walichokaa madiwani wakakubalina, hivyo muda ukifika watajiondoa wenyewe ", alisema Kanyasu .

Aidha katibu wa umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi, UVCCM wilayani Geita Bw Rajab Ally  Rajab akitoa salaam za chama hicho kwenye mkutano huo alipinga hatua ya mkurugenzi huyo na kusema kuwa serikali haiwezi kuwazuia waendesha Baiskeli hao kutoa huduma hiyo mjini bila kuwaandalia mazingira ya eneo la kutolea huduma hiyo na kwamba chama hicho hakiko tayari kuona vijana wanahangaika .

"Wanaofanya kazi ya kuendesha daladala za baiskeli wengi ni vijana na ni wapiga kura  wa chama change, Chama hakiwezi  kukubali watimuliwe mjini watafanyia kazi zao wapi bila kuwaandalia mazingira? Mkurugenzi hakukishirikisha chama tulishituka baada ya kusikia matangazo", alisema katibu Ally  Rajabu.


Hivi karibuni mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya mji wa Geita aliwatangazia waendesha daladala za baiskeli kusitisha kutoa huduma ya kubeba abiria mjini na badali yake wafanye shughuli zao kwenye maeneo ambayo walikuwa wamepangiwa yakiwemo ya Nyankumbu na Mwatulole pembezoni mwa  mji  kwa madai kuwa wamekuwa chanzo cha ajali za barabarani mjini hali iliyosababisha kuibua maandamano makubwa  ya waendesha daladala hadi katika ofisi za mbunge wa jimbo la Geita mjini .

No comments:

Post a Comment