Monday 7 November 2016

WANANCHI WILAYANI GEITA WAOMBWA KUENDELEA KUCHANGIA MADAWATI













Mkuu wa wilaya Mwl Herman Kapufi  akitoa maagizo kwa wanafunzi kuakikisha wanatunza madawati hayo ili yaje yawafae kwa baadae.



Mkuu wa wilaya ya Geita,Herman Kapufi akikabidhi madawati kwa mkurugenzi wa halmashauri ya Mji pamoja na baadhi ya wanafunzi.



Bwn.Shokerela na mke wake wakifurahia baada ya kuwa wamekabidhi madawati kwa mkuu wa wilaya ya Geita.

Jamii  na Mashirika Mbalimbali Wilayani na Mkoani Geita, yameombwa kuendelea  kujitolea kuchangia Madawati  ili kunusuru  Wanafunzi kuendelea kukaa chini pindi wanapokuwa  masomoni.
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Geita Mwl.Herman  Kapufi  wakati alipokuwa akikabidhiwa Madawati 14  yaliyotolewa na familia  ya ndugu  Shokelera.

Amesema kuwa  Wanafunzi walioandikishwa ni wengi sana kwenye Wilaya hiyo  hivyo wengi wamejikuta wakikaa  chini   madarasani na kushindwa kuelewa kile ambacho  wanafundisha pindi  wanapokuwa Madarasani huku akiwataka wale  wote waliotoa Ahadi kutekeleza  kile  walicho ahidi.
Aidha kwa upande  wake Afisa Elimu Msingi Halmashauri  ya Mji ,Bi.Catherine  Mashala ameelezea kuwa Madawati hayo 14 ambayo yametolewa yatapelekwa shule ya msingi Kalangalala iliyopo Wilayani hapa.

Kwa upande wake Bw.Panklas Shokerela, amefafanua kuwa wamekabidhi Madawati hayo kutokana na Ahadi ambayo walitoa siku ya Uchangiaji  wa Madawati na kwamba Lengo la kukabidhi ni kuunga Mkono Jitihada za Rais Magufuli  za kutaka Watoto wasome katika Mazingira yaliyo bora.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita, Mhandisi Modest  Apolinary amewashukuru  Wadau ambao  wameendelea kujitolea kuchangia Madawati  katika Halamshauri  hiyo.

No comments:

Post a Comment