Monday 20 March 2017

BAADHI YA WAFANYABIASHARA WA SOKO LA CCM MKOANI GEITA WAONDOLEWA



Baadhi  ya akina mama wanao fanya biashara katika soko linalo milikiwa na chama cha mapinduzi (CCM)  katika mamlaka ya mji mdogo wa katoro wilayani na mkoani Geita wamelalamikia uongozi wa eneo hilo kwa kuwavunjia meza zao za biashara kwa madai ya kuto lipa kodi .
Tukio hilo limetokea march 18, 2017 ambapo jumla ya meza nne zimeondolewa katika soko hilo kwasababu zinazo elezeka kuwa kina mama hao wameshindwa kulipa  pango la  ardhi katika soko hilo.
wakizungumza kina mama hao ambao wanatambulika kwa majina ya Agnes Gervas, Pendo Kayanda, Agnes Juma na Lusia Lukas wamesema kuwa utaratibu wa kulipa kodi katika eneo hilo huwa wanalipa kila ifikapo tarehe 20 ya mwezi wa 4 lakini imekuwa tofauti kwa mwaka huu ambapo wametakiwa kulipia meza hizo mwezi wa tatu mwaka huu.

Aidha wameiomba Serikali kuwatengea eneo la kufanyia shughuli zao za kibiashara kutokana na kunyanyaswa katika soko hilo

Kwa upande wake msemaji wa kamati ya soko hilo Rashid Shaka amesema kuwa utaratibu wa ukusanyaji kodi umebadilika na taarifa za mabadiliko hayo zilifikishwa kwa wafanya biashara wote kabla ya utekelezaji  wa ukusanyiaji mapato kuanza.


Naye mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi  kata ya Katoro  Philimoni Mgoyezi ameeleza kuwa taarifa za kuondolewa kina mama hao amezipata na ameiomba kamati husika kutotumia nguvu kubwa kwa wafanyabiashara katika soko hilo na badala yake watumie busara wakati wa kutatua migogoro  inayo jitokeza.

No comments:

Post a Comment