Wednesday 22 March 2017

SERIKALI MKOANI GEITA YAWAASA WANACHI KUTOA USHIRIKIANO DHIDI YA VITENDO VYA UKATILI



Serikali mkoani geita imewataka wananchi kuwafichua watu wanajihusisha na vitendo vya ukatili kwa watoto wadogo waishiyo katika mazingira magumu  kwani kwa kufanya hivyo nikuwasaidia watoto  kutoka katika wimbi hilo ambalo limekuwa likiwapatia wakati mgumu.
Hatua hiyo imekuja mara baada ya mtoto mdogo anaekadiliwa kuwa na umri wa kuanzia miaka kumi ambaye anatambulika kwa jina la Nestori Safari mkazi katika mamlaka  ya mji mdogo wa katoro amejikuta katika wakati mgumu ambapo ndugu aliye kuwa akiishi nae kamfanyia ukatili wa kinyama.
Akizungumza mtoto huyo amesema kuwa kitendo hicho alifanyiwa na jirani yake ambae alikuwa akiishi nae ambapo alimfunga manati kwenye mikono yake miwili kisha kuanza kumuadhibu hadi kupelekea mikono hiyo kufikia hatua ya kuoza kwasababu ya kukaa muda mrefu ikiwa na majeraha kutokana na hilo mtoto huyo anaiomba serikali pamoja na watu wenye moyo wa huruma waweze kumsaidia kwani hali yake siyo nzuri.

Mtoto huyo amesema baba yake alifariki kwa kupigwa na wananchi kwa kusadikika kuwa ni mwizi lakini mama yake yupo lakini amesha changanyikiwa kiakili kwahiyo muda wote amekuwa akishinda katika vilabu vya pombe za kienyeji na amekuwa hana msaada wowote kwake.

Kwa upande wake Kamanda wa jeshi la jadi sungusungu katika mtaa wa Ibozya Magigo  kata ya katoro ambapo mtoto huyo anaishi Bw. Hamisi Twaha  amesema kuwa watu wamrudie mungu kwani kitendo hicho nicha kikatili na hakifai katika  jamii kwani mtoto huyo inaweza kupelekea kukatwa mikono yake yote miwili kutokana na mikono hiyo kuanza kuoza.

Kamanda huyo amesema mtuhumiwa mpaka sasa ameshafikishwa katika kituo cha polisi  katoro kwa uchunguzi zaidi.


Aidha mwenyekiti wa mtaa huo wa Ibozyamagigo Bw. Mapambano Pasikali amelaani kutokea kwa kitendo hicho na amewaomba watu wenye kuguswa na jambo hilo wajitokeza kumchangia mtoto huyo kwani hali aliyo nayo  ni mbaya sana 

No comments:

Post a Comment