Tuesday 20 June 2017

MBUNGE WA JIMBO LA BUKOMBE DOTTO BITEKO APOKELEW KWA SHANGWE






Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto  Mashaka Biteko  amewaomba wananchi wa Jimbo lake kuwa na Imani naye kwani yeye ndiye mwakilishi wao kwa sasa  huku akiwaomba na kuwasihi wazidi kumuombea Rais Magufuli kwa kazi ngumu anayoifanya ya kuwatetea wanyonge pamoja na maslahi ya Taifa kwa ujumla.
Biteko amebainisha hayo katika mkutano wake wa kuwashukuru wananchi wa Jimbo hilo la Bukombe kwa kumuwezesha kumchagua kwa  kura nyingi na pia kumpigia Rais Magufuli kwa kula za kutosha kuingia madarakani.

Aidha,Doto aliwaomba wananchi wa Kata Bulangwa  kuwa na subira kwani atahakikisha Umeme wa gridi ya Taifa inapita katika vijiji vyote vya Wilaya ya Bukombe uku akiwabainishia mradi uliokwisha haukua  Mradi wa REA hivyo amewaeleza mpango wa sasa ni kupata umeme wa uhakika hadi kwenye baadhi ya vyanzo vya maji ili kupunguza na changamoto ya maji na kwa sasa tayari ameliombea hilo na litatekelezwa muda wowote kuanzia sasa.

Mbali na hilo pia aliwataka wananchi wa Jimbo hilo la Bukombe  kutojenga katika miundo mbinu ili wakati wa serikali kufanya maendeleo kusiwe na kikwazo cha kuwaathiri wananchi hao. 

 Mhe. Doto Mashaka Biteko pia mbali na kutoa shukrani kwa wapiga kula wake hao, pia alipata wasaha wa kusikiliza kero za wananchi huku akipokea kero zao hizo ambapo ameeleza kuwa atazifanyia kazi

Wananchi waliuliza maswali mbalimbali ikiwemo ukosefu wa maji,kusumbuliwa na wahifadhi na kuuliza nini hatima ya serikali juu ya milioni hamsini za kila kijiji, barabara mbovu pamoja na Ukosefu wa Umeme.

No comments:

Post a Comment