Jeshi la Polisi nchini
limetamba kushinda vita dhidi ya uhalifu baada ya kupunguza matukio ya aina
hiyo huku likikiri kuongezeka kwa vitendo vya ubakaji na kunajisi.
KUHABARISHA NA KUFAHAMISHA KUHUSU HABARI NA MAMBO YANAYOENDELEA KATIKA JAMII YA GEITA, KANDA YA ZIWA, TAIFA NA DUNIANI. TUTUMIE HABARI AU WASILIANA NASI KUPITIA info@stormfm.co.tz au +255 685 883 870
Thursday, 21 December 2017
Tuesday, 19 December 2017
DAKTARI FEKI ANASWA HOSPITALI YA MKOA WA MWANZA
Jeshi la polisi mkoani
Mwanza linamshikilia mtu mmoja kwa kosa la kujifanya daktari, katika hospitali
ya mkoa Sekou Toure.
TAARIFA YA CHADEMA JUU YA UTEUZI WA MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA SINGIDA KASKAZINI
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) amesikika asubuhi
hii wakati akihojiwa na Radio Clouds Fm kwenye kipindi cha Power Breakfast,
akisema kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimechukua fomu za
kugombea ubunge katika uchaguzi wa marudio Jimbo la Singida Mashariki, mkoani
Singida.
Kupitia taarifa hii ya awali, tungependa vyombo vya habari na
umma kwa ujumla ujue kuwa;
1. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) hakijateua
mgombea kuwania nafasi ya ubunge katika uchaguzi huo wa marudio, Jimbo la
Singida Kaskazini.
2. Mkurugenzi wa NEC, Ndugu Ramadhan Kailima atambue kuwa suala
la kugombea nafasi ya ubunge kwa mchakato wa ndani ya CHADEMA linasimamiwa na
Kamati Kuu ya Chama na hivyo hivyo yeye hana mamlaka wala hawezi kuwa msemaji
wa suala hilo katika hatua ya sasa.
3. Tunafuatilia kupata taarifa za kina kuhusu msingi wa kauli ya
Mkurugenzi hiyo, kisha tutatoa taarifa kamili katika hatua ya baadae.
Imetolewa leo Jumanne, Desemba 19, 2017 na;
Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
Monday, 18 December 2017
VODACOM TANZANIA FOUNDATION, DORIS MOLLEL FOUNDATION WATOA MSAADA WA VIFAA TIBA VYENYE THAMANI YA SH ,MILIONI 24 KWENYE HOSPITALI YA WILAYA YA CHATO, GEITA
Baadhi ya vifaa tiba ambavyo vimetolewa kwenye hospitali ya Wilaya ya Chato Mkoani Geita ambavyo vitaweza kuwasaidia watoto ambao wanakuwa bado hawajafikia muda wa kuzaliwa. |
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Chato,Dkt. Ligobert Kalasa akitoa maelezo ya namna ambavyo mashine hizo zinatumika. |
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Afya), Dkt. Mpoki Ulisubisya akitoa maelezo juu ya kitanda cha wagonjwa ambacho kilikuwa nje ya hospital. |
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia akimsalimia mmoja wa watoto waliozaliwa katika Hospitali ya Chato, Mkoani Geita leo. |
KINANA ASEMA YUPO TAYARI KUITUMIKIA CCM....ATOBOA SIRI YA USHINDI WA KISHINDO
Katibu Mkuu wa Chama
cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana amesema yuko tayari kuendelea
kukitumikia chama hicho.
“Neno la mwenyekiti kwangu ni amri
kama umeona bado unahitaji niendelee kukusaidia niko tayari kufanya hivyo,”
alisema Kinana leo Jumatatu Desemba 18,2017 katika mkutano mkuu wa CCM
unaoendelea mjini Dodoma.
Kinana ametoa kauli
hiyo wakati kukiwa na minong’ono kuwa ameandika barua akiomba kuachia nafasi
yake ya ukatibu mkuu.
Awali, Mwenyekiti wa
CCM, Rais John Magufuli aliweka wazi kuwa Kinana amekuwa msaada mkubwa katika
kukiongoza chama hicho.
“Mzee Kinana
amenisaidia sana. Amenisaidia mno kwenye kufanya mabadiliko ndani ya chama na
ni mategemeo yangu ataendelea kunisaidia,” alisema.
Katika hatua nyingine,
Kinana ametoa siri ya ushindi wa kishindo wa chama hicho katika uchaguzi kuwa
ni kutokana na ilani bora, demokrasia na kusikilia maoni ya wanachama.
Kinana amesema
demokrasia imekuwa msingi wa chama hicho ndiyo sababu kinaimarika.
“CCM tunazingatia
demokrasia, wanachama wapo huru kutoa maoni ndani ya chama. Hili linafanyika
kwa kuwa usipowapa uhuru wa kusema ndani watasema nje,” alisema.
SERIKALI MKOANI GEITA YAJIPANGA KUTATUA TATIZO LA MAJI KWA WANANCHI
Eneo la mitambo ya uzalishaji wa maji ambayo hipo kijiji cha Nungwe. |
Fundi wa mitambo ya maji kutoka mgodi wa dhahabu wa Geita,(GGM)Denis Domician akitoa maelezi namna ambavyo maji yamekuwa yakitibiwa kabla ya kusambazwa kwa watumiaji mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Geita. |
Fundi wa mitambo ya maji kutoka mgodi wa dhahabu wa Geita,(GGM)Denis Domician akitoa maelezo namna ambavyo maji yamekuwa yakipita na kutibiwa kwenye sehemu ambazo zimetengwa. |
Eneo la kutibia maji. |
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Gabriel pamoja mhandisi wa maji wa Geuwasa wakitoa maelezo ya namna ambavyo Tanki hilo limekuwa kikifanya kazi wakati alipotembelea kwenye tanki hilo. |
Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Geita,Mhandisi Modest Aporinal akitoa maelezo ya namna ambavyo wanatarajia kupitisha mabomba kwenye mtaa wa 14 kambarage kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita. |
Friday, 15 December 2017
SPIKA WA BUNGE AAHIDI KWENDA NAIROBI KUMTEMBELEA TUNDU LISSU
Spika wa Bunge,
Mhe. Job Ndugai amefunguka na kusema atakwenda jijini Nairobi nchini
Kenya kumuona Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu ambaye anafanyiwa
matibabu katika hospitali ya Nairobi nchini Kenya kufuatia kupigwa risasi
Septemba 7, 2017.
Wednesday, 6 December 2017
NAIBU WAZIRI MAZINGIRA ASWEKA NDANI VIGOGO WATANO MKOANI GEITA KUTOKANA NA UKIUKWAJI WA SHERIA ZA MAZINGIRA
Moja kati ya wakurugenzi wa Mgodi wa Nyarugusu Mine Co.Limited Fred Masanja akionesha cheti NEMC ambacho naibu waziri alikikata. |
Bwawa la kuhifadhia maji ya kemikali ambalo limeharibika na kusababisha maji mengi kuelekea kwenye shughuli za wananchi. |
Naibu Waziri wa Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Rais Inayoshughulika na muungano na Mazingira Mheshimiwa Kangi Lugola akiangalia baadhi eneo ambalo limepasuka. |
Naibu Waziri wa Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Rais Inayoshughulika na muungano na Mazingira Mheshimiwa Kangi Lugola ,akitembelea na kuangalia miche ya miti ambayo imekwisha kuathirika. |
Tuesday, 5 December 2017
MGODI WA DHAHABU WA GGM MABINGWA MICHEZO YA SHIMMUTA
Subscribe to:
Posts (Atom)