Thursday 23 November 2017

RC GEITA MHANDISI LUHUMBI AWATAKA WANANCHI KUONGEZA JUHUDI KATIKA UJENZI VITUO VYA AFYA SHULE

DSC_0424
Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufu akishiriki zoezi la ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Kasota.

DSC_0427
Wananchi wakishiriki zoezi zima la ujenzi wa zahanati.

DSC_0436
Mganga Mkuu wa wilaya ya Geita Dkt Raphael Mhina akishiri zoezi la ujenzi wa zahanati kwenye kijiji na kata ya Kasota.

DSC_0454
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akisisitiza wananchi kuendelea kujitokeza kwenye shughuli za maendeleo.

DSC_0560

DSC_0562

DSC_0581
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akishiriki ujenzi wa madarasa shule ya msingi Ludete(Picha na Joel Maduka)

Mkuu wa mkoa wa Geita Mhandisi Robert Luhumbi ameendelea na za ujenzi wa vyumba vya madarasa pamoja na zahanati kwenye kata za Ludete na Kasota lengo likiwa kupunguza changamoto za kimiundombinu zinazoukabili Mkoa huo ambao ameutaja kuwa wa mwisho katika suala hilo

Akizungumza na  wakazi wa Kata ya Ludete Wilayani Geita , Mhandisi Luhumbi alisema wananchi wana moyo wa kujitoa na kutaka maendeleo lakini wanakwamishwa na ukubwa wa gharama za wakandarasi kwenye baadhi ya miradi

“taarifa nilizozipata ni mbaya katika mkoa wetu mkoa huu niwa mwisho katika mambo ya miundo mbinu takwimu  hizi ziliniamsha nisikae ofisini nina mikakati ya kuhakikisha zahanati zinajengwa kwa kila kijiji ,mitaa na hata kata ’’Alisema Luhumbi

 Luhumbi alisema baadhi ya watendaji wamekuwa wakitumia miradi ya maendeleo kujinufaisha na kutaka bei elekezi ya gharama za ujenzi itolewe ili wananchi wajenge miradi yao na fedha ziwanufaishe wananchi husika

“nimegundua wananchi wanamoyo wa kujitolea lakini waanaangushwa na wakandalasi gharama nikubwa mno ambayo wanakutana nayo alafu miradi haikamiliki kuanzia wakati huu tutatoa bei elekezi na mkandalasi ni marufuku kwa Mkoa wa Geita kwa majengo ya shule madarasa watajenga wananchi husika’’


Mhandisi Luhumbi amewapongeza wananchi kwa jitihada zao na kwamba bado Serikali inahitaji juhudi zao huku akiwahakikishia kuwa ofisi yake itashirikiana nao ili kuondoka kwenye nafasi ya mwisho katika masuala ya Kimiundombinu

No comments:

Post a Comment