
Serikali kupitia Mfuko
wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) unakamilisha taratibu za uwekeza kwenye vifaa
tiba vitokanavyo na pamba na bidhaa za maji ya dripu(Infusion Fluids).
Hayo yamesemwa leo na
Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles Mwijage wakati akijibu hoja
mbalimbali za wabunge mjini Dodoma.
“Gharama za miradi hii
inakadiriwa kufikia dola za kimarekani milioni 36.5 na kutoa ajira za moja kwa
moja 1600 na zisizo za moja kwa moja 5000”, Alisema Mhe.Mwijage.
Amesema mradi huu
unakadiriwa kutumia pamba tani elfu 50 kwa mwaka na Serikali ya Mkoa wa Simiyu
inaendelea na jitihada za kutenga maeneo ya uwekezaji kwa kuwalenga
wajasiriamali wadogo,wa kati mpaka wakubwa bila kujali kama ni wa kutoka ndani
au nje ya nchi.
Aidha amesema kuwa
azma ya Serikali ya ujenzi wa uchumi wa viwanda imeainishwa vyema katika mpango
wa pili wa Maendeleo wa miaka mitano wa mwaka 2016/17-2020/21 wenye dhima ya
kujenga uchumi wa viwanda ili kuleta mageuzi ya kiuchumi na maendeleo ya watu.
Pamoja na hayo
ameainisha kuwa ili kufikia azma hiyo ushiriki wa mchango wa mtu mmoja
mmoja,makundi ya watu,taasisi za umma na taasisi binafsi unahitajika.
Amebainisha
mikakati minne ambayo imeanza kufanyiwa utekelezaji ni ya ngozi,mafuta ya
kula,nguo na mazao jamii ya kunde uku wakati huohuo mpango wa wilaya moja,zao
moja na uhamasishaji wa ujenzi wa viwanda chini ya SIDO unaendelea nchini kote.
No comments:
Post a Comment